Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Konkoni amchomoa kiungo Yanga

STRAIKA mpya wa Yanga, Hafiz Kankoni ameanza mambo huko Avic Town baada ya kutupia bao moja juzi wakati timu hiyo likiichapa Friends Rangers mabao 6-1, lakini kama ulikuwa haujui, ujio wa Mghana huyo umemmng’oa kiungo kikosini.

Iko hivi. Baada ya kuondoka kwa Mkongomani Fiston Mayele, Yanga iliingia sokoni kutafuta mrithi wake lakini zoezi hilo likawa gumu ikafika muda vigogo wa timu hiyo wakakaribia kukata tamaa ili wawaachie mikoba Clement Mzize na Kennedy Musonda.

Wakati huo huo, Yanga walimrejesha kikosini kiungo Mrundi Gael Bigirimana aliyechomolewa dirisha dogo la msimu uliopita na nafasi yake kuchukuliwa na Mamadou Doumbia ambaye pia ameachwa mwishoni mwa msimu uliopita.

Bigirimana alifika kambini Avic na kuanza kupiga tizi akiendelea kuutumikia mkataba wake wa miaka miwili, lakini ghafla alipigwa ‘stop’ baada ya Yanga kumpata Kankoni kwani straika huyo Mghana alifanya chama hilo kufikisha mastaa wa kigeni 12. Mwanaspoti limepenyezewa na mmoja wa watu wa karibu na Bigirimana, baada ya kuambiwa hivyo waliongea na mabosi wa Yanga na kuamua kuvunja mkataba jumla baada ya kufanyiwa hivyo mara mbili.

“Sasa tumechoka, alifanyiwa hivi msimu uliopita na sasa. Tumeamua kuvunja mkataba na tayari viongozi wa Yanga wanalijua hilo na wanalifanyia kazi,” alisema mtu huyo wa Bigirimana alipozungumza na Mwanaspoti lililoulizia ujio wa kiungo huyo wa zamani wa Newcastle United ya England. Yanga leo itasafiri kwenda tanga tayari kwa mechi za ngao ya Jamii ambapo itarusha karata yake ya kwanza Agosti 9 dhidi ya Azam na kama itashinda au kufungwa itarudi tena uwanjani Agosti 13 kuvaana na Simba au Singida Fountain Gate.