Macho yote Ujerumani leo

Munich, Ujerumani. Michuano ya Kombe la Euro inaanza leo nchini Ujerumani, huku mechi kali ambayo inasubiriwa kwa hamu kubwa ikiwa kati ya Ujerumani na Scotland.

Hii ni mechi ya Kundi A ambayo itaanza kwa kuonyesha picha halisi ya michuano hiyo msimu huu itakavyokuwa ikiwa inapigwa kwenye Uwanja wa kisasa wa Munich Football Arena.

Mashabiki wa Ujerumani hawana matumaini makubwa na timu yao kutokana na kushindwa kufanya vizuri kwenye michuano kadhaa iliyopita ya hivi karibuni.

Hata hivyo, mara mbili nyuma Ujerumani imeshindwa kufanya vizuri kwenye michuano hii baada ya kutolewa kwenye hatua ya makundi mara mbili kati ya tatu za hivi karibuni, hivyo msimu huu wanataka kuvunja mwiko huo.

Ujerumani ni kati ya taifa ambalo limefanya vizuri kwenye michuano hii ikiwa imeshatwaa ubingwa mara tatu ikiwa sasa inakwenda kuutafuta kwa mara ya nne ikiwa kwenye aridhi ya nyumbani.

Kocha kijana Julian Nagelsmann hakuanza vizuri kikosi hicho, lakini baada ya kuibuka na ushindi kwenye michezo dhidi Ufaransa na Uholanzi kwenye michezo iliyopigwa mwezi Machi imeanza kuonyesha mwanga halisi wa kikosi hicho.

Hata hivyo Scotland imetengeneza kikosi chake baada ya kuonyesha uwezo mkubwa kwenye michezo ya kufuzu baada ya kuibuka na ushindi dhidi ya mataifa makubwa Hispania, Norway na  Georgia.

Mbali na kuwa na kikosi imara, lakini timu hiyo ipo chini ya mwanafuzi wa Jose Mourinho Steve Clarke ambaye amefanikiwa kuunda kikosi imara chenye kasi na maarifa ya hali ya juu kwenye eneo la ulinzi.

Imekuwa timu ambayo inamtegemea zaidi nahodha wa Aston Villa  John McGinn na kiungo wa Manchester United Scott McTominay pamoja na beki wa Arsenal  Kieran Tierney.

Kiungo huyo wa United ndiye alikuwa mhimili wa timu hiyo kwenye harakati za kufuzu baada ya kufunga mabao mabao saba kwenye mechi nane za kufuzu.

"Mashindano haya nchini Ujerumani yanaonekana kuwa yatakuwa bora sana Timu ya taifa ya Ujerumani ni kati ya zile ambazo ni hatari zaidi kwenye soka la Ulaya, tunatarajia mchezo mgumu, lakini naamini kuwa nasi tutaipa mechi ngumu sana, tupo tayari kwa ajili ya mchezo huu na kila mmoja atafurahia,” alisema Steve Clarke .

Ujerumani itakuwa inategemea kiwango cha mastaa wake wawili ambao wametwaa ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Ulaya hivi karibuni wakiwa na Real Madrid Ton Kroos na Rudiger, lakini pia ikiwa chini ya wakongwe Manuel Neuer na Kimmich.

Safu ya ushambuliaji ya timu hiyo itaongozwa na mshambuliaji wa Arsenal Kai Havertz.

Huku kocha mkuu wa timu hiyo akiwa na hofu na kasi ya Scotland kwa kuwa ni kati ya timu yenye vijana wengi.

Hii ni mara ya pili Ujerumani inaandaa michuano hii ya Ulaya kwangu pamoja na wachezaji wangu tunatakiwa kuhakikisha tunabakiza.

“Kuna presha kubwa, lakini nataka kuwahakikishia kuwa tupo tayari kupambana kwa hali yoyote ile, mashabiki watarajie michuano bora sana.