Maguire alia Man United kunyimwa penalti

Muktasari:

  • Mechi nne nyumbani bila ushindi wala kufunga bao kwenye Uwanja wa Anfield kwa dakika 348, na sasa Manchester City wanakutana na Manchester City, Jumapili.

Manchester, England. Mechi nne nyumbani bila ushindi wala kufunga bao kwenye Uwanja wa Anfield kwa dakika 348, na sasa Manchester City wanakutana na Manchester City, Jumapili.

Harry Maguire amesisitiza kuwa angetakiwa kuzawadiwa mkwaju wa penalti dhidi ya West Bromwich Albion katika mchezo wa juzi wa Ligi Kuu England.

Lakini mchambuzi wa soka, Graeme Souness, alimshutumu nahodha huyo wa Manchester United kwa kujirusha ili kupata penalti kwenye mchezo huo.

Mashetani Wekundu walijikuta wakijizamisha shimoni wenyewe katika mbio za ubingwa kwenye Uwanja wa The Hawthorns, wakati Mbaye Diagne akifunga kwa kichwa kilichomshinda kipa David de Gea, dakika ya pili ya mchezo.

Bruno Fernandes aliisawazishia Man United dakika moja kabla ya timu kwenda mapumziko, licha ya kuwa kikosi cha kocha Ole Gunnar Solskjaer kilishindwa kutengeneza nafasi za kufunga.

Maguire, ambaye sasa ana miaka 27, alidhani kuwa ameipatia timu yake nafasi ya kupata bao la ushindi, lakini alioonekana kuvutwa na kuangua ndani ya eneo la hatari na beki wa Baggies, Semi Ajayi.

Beki huyo wa kati aliiambia Sky Sports mara baada ya mchezo huo kumalizika: “Nilikuwa na uhakika kabisa kuwa ile ilikuwa penalti. “Sikuelewa kwanini mwamuzi (Craig Pawson) aliambiwa kuwa ana haja ya kwenda kuangalia mwenyewe katika ile tv ya uwanjani.

“Nilikuwa ndani ya eneo la penalti na nilihisi kuna mtu ananigusa begani, alikuwa ananivuta kwa nyuma na pia kulikuwa na mgusano wa miguu ulionifanya nianguke.

“Haikuwa mbaya lakini ilikuwa penalti. Hasa baada ya mwamuzi kuonyesha kuwa ilikuwa penalti, nilihisi kuwa hakukuwa na sababu ya kuwa na uamuzi wa tofauti tena na niliamini ilikuwa tumepata penalti.

“Lakini baada ya muda ikaonekana uamuzi ulitubadilikia. lakini tulishafanya makubwa kushinda mchezo, hatutakiwi kutegemea uamuzi wa VAR, tulitakiwa kufanya zaidi uwanjani.

“Tulifanya makubwa katika kushambulia na kutengeneza nafasi za kupata ushindi bila mafanikio, lakini bado tunatakiwa kufanya makubwa zaidi.”

Katika studio za Sky Sport, Souness alikuwa na mawazo tofauti katika tukio alilokuwa akililalamikia Maguire.

Mchambuzi huyo alisema: “Alianguka kama mtu aliyepigwa kikumbo na mchezaji wa baseball, ulikuwa uamuzi wa kijinga wa kujiangusha.”

Kama ilivyoonekana katika picha za marudio, ilionekana kama aliyechezewa vibaya, lakini kabla ya tukio hilo, Maguire alionekana kuwa ameshaotea.

Lakini tukio hilo lilishindwa kuonekana haraka... ikiwa na maana kuwa uamuzi wa awali wa penalti ulitakiwa kubaki, lakini mwamuzi Pawson aliamua kujiridhisha kwa kuangalia katika tv ya uwanjani. Lakini mwishoni mwa mchezo, West Brom ilifanikiwa kuondoka na pointi moja baada ya mchezo kumalizika kwa sare ya bao 1-1, jambo ambalo limewaacha bao nyuma ya mstari wa kushuka daraja kwa pointi 12, ikiwa nafasi ya 19.

Man United, kwa upande wake ilishindwa kutumia nafasi hiyo kusogea kileleni ikipunguza pointi dhidi ya Manchester City, ikiwaacha majirani zao wakitamba kwa pointi saba zaidi kileleni.