Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Majeraha ya Gabriel yaitisha Arsenal

London, England. Arsenal watalazimika kusubiri kwa wasiwasi baada ya Gabriel Magalhães kutolewa uwanjani na Brazil kutokana na jeraha wakati wa mechi ya kirafiki dhidi ya Senegal.

Beki huyo mrefu wa kati, ambaye yuko katika kiwango bora zaidi cha maisha yake kwenye kikosi cha The Gunners, alishika sehemu ya nyonga baada ya kutolewa na Carlo Ancelotti katika mchezo uliochezwa usiku kwenye Uwanja wa Emirates.

Alionekana kuwa na maumivu baada ya kugongana dakika ya 63 kwenye mchezo huo uliochezewa Kaskazini mwa London, uwanjani ambako ametoa kiwango cha juu sana msimu huu akiwa na klabu yake.

Akiwa ameandamana na wahudumu wa afya, Gabriel alitoka uwanjani kwa hatua za polepole huku akionekana mwenye huzuni wakati akifanyiwa mabadiliko na Wesley, beki wa Roma.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 alipokelewa kwa makofi mengi kutoka kwa mashabiki, lakini mara moja aliingia kwenye mazungumzo na madaktari wa timu ya taifa alipokuwa akiondoka uwanjani.

Hali hii inampa hofu Mikel Arteta, ambaye anaweza kumpoteza beki wake mwenye kiwango kizuri kuelekea michezo mikubwa dhidi ya Tottenham, Bayern Munich na Chelsea katika wiki zijazo.

Gabriel Magalhães alitolewa na Brazil kutokana na jeraha wakati wa mchezo dhidi ya Senegal.

Beki huyo wa kati alishika sehemu ya nyonga kwa maumivu alipokuwa akitembea nje ya uwanja akiwa na madaktari.

Marquinhos, beki wa PSG, aliashiria kwa benchi kwamba Gabriel alihitaji kubadilishwa baada ya kugongwa.

Mchezaji huyo alikuwa sehemu ya ushindi mzuri wa 2-0 wa Brazil, ushindi mwingine katika mfululizo wa mechi za taifa hilo zilizofanyika kwenye uwanja wa Emirates.

Seleção tayari wamefuzu Kombe la Dunia na walikuwa wakicheza mechi ya kirafiki dhidi ya Senegal, huku ushiriki wa Gabriel ukitarajiwa kuwapa furaha mashabiki wa Arsenal waliotaka kumwona.

Lakini sasa beki huyo anakabiliwa na hatari ya kuwa nje kwa kipindi fulani, baada ya msimu huu kuuanza akitoka kwenye jeraha la misuli ya paja (hamstring) alilopata Aprili na lililomweka nje kwa miezi kadhaa.

Gabriel amekuwa muhimu kwenye uimara wa safu ya ulinzi ya Arsenal msimu huu, akisaidia timu kupata clean sheet saba katika mechi 11. Pia ameendelea kuwa tishio mbele, tayari akifunga mabao mawili kwa kikosi cha Arteta.

Mechi ya Brazil dhidi ya Senegal ilikuwa mara ya tisa kwao kucheza katika Uwanja wa Emirates. Taarifa kwenye tovuti ya Arsenal wiki iliyopita ilielezea uwanja huo kuwa “nyumbani kwa Brazil, wakiwa ugenini”.

Taarifa hiyo inaongeza: “Seleção wamekuwa na uhusiano wa karibu na uwanja wetu tangu tuhamie kutoka Highbury mwaka 2006 na wamekabiliana na mataifa mbalimbali kutoka penjew za dunia katika kipindi hicho.”