Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Makala: Kamati za Tenga batili

Muktasari:

  • Uchaguzi Mkuu wa TFF uliopangwa kufanyika mwezi Februari ulisimamishwa kutokana na baadhi ya wagombea kupinga kuenguliwa na baadaye kwenda Fifa.

Dar es Salaam. Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Amos Makala amemshangaa Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Leodegar Tenga kutangaza kamati mpya za TFF wakati katiba yake haijapitishwa na Msajili wa Vyama vya Michezo nchini.

Akizungumza na gazeti hili kwa njia ya simu, Waziri Makala alisema kamati zilizotangazwa hivi karibuni na Tenga ni batili.

“Katiba ya TFF mpaka sasa haijapitishwa na Msajili kwa vile ina upungufu mwingi na moja ya upungufu huo ni kwamba haionyeshi  vipengele vilivyopitishwa kama vilipigiwa kura, na kama vilipigiwa kura idadi ya waliopiga kura za ndiyo ni wangapi na waliokataa ni wangapi, imepitishwa tu kienyeji,”alisema Makala.

“Nawashangaa sana TFF wametangaza kamati zao mpya wakati katiba haijapitishwa, hizo kamati walizozitangaza ni batili na hatuzitambui, wanatakiwa wafuate taratibu, wametangaza kamati kwa katiba ipi? Wangesubiri katiba ipite ndiyo watangaze kamati zao, sasa wao wametangaza kamati wakati katiba yao ina upungufu.

Makala alisema bado Msajili wa vyama vya Michezo anaishughulikia katiba hiyo ya TFF na muda wowote kuanzia sasa atairudisha TFF ili ifanyiwe marekebisho.

Akizungumzia kauli hiyo ya naibu waziri, Katibu wa Mkuu wa TFF, Angetile Osiah alisema wao hawajapata taarifa rasmi ya suala hilo.

“Bado hatujapokea taarifa rasmi ya suala hilo,” alijibu Osiah kwa kifupi.

Kufuatia hali hiyo uchaguzi wa TFF ambao ulipangwa kufanyika Septemba 29 kama ilivyoagizwa na Fifa sasa upo kwenye hatihati kufanyika kwa wakati.

Rais Tenga alitangaza kamati hizo mwezi uliopita ambazo wajumbe wake ni kama ifuatavyo:

Kamati ya Rufaa za Maadili ni Jaji Steven Ihema (mwenyekiti), Victoria Makani (m/mwenyekiti), Mhe. Mohamed Misanga, Henry Tandau na Mhe. Murtaza Mangungu.

Kamati ya Maadili:  Jesse Mguto (mwenyekiti), Francis Kabwe (m/mwenyekiti), ACP Mohamed Mpinga, Prof. Madundo Mtambo, na Evod Mmanda.

Kamati ya Rufaa na Nidhamu: Prof. Mgongo Fimbo(mwenyekiti), Ong’wanuhama Kibuta (m/mwenyekiti).

Kamati ya Nidhamu: Kamanda Mstaafu Alfred Tibaigana (mwenyekiti), Mustafa Kambona (m/mwenyekiti), Azzan Zungu, Yussu Nzowa.

Kamati ya Rufaa za Uchaguzi: Jaji Bernard Luanda (mwenyekiti), Francis Kiwanga (m/mwenyekiti)

Kamati ya Uchaguzi: Hamidu Mbwezeleni (mwenyekiti), Moses Kaluwa (m/mwenyekiti), Mustafa Siani, Hassan Dyamwale na Kitwana Manara.

Kamati ya Waamuzi: Kapteni Mstaafu Stanley Lugenge (mwenyekiti), Omar Kasinde (m/mwenyekiti)