Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Makosa 22 yaliyosababisha Onana kuondoka Man United

ONANA Pict

Muktasari:

  • Baada ya kushuhudia makosa inaeleweka wazi kwanini Man United imechoshwa na kipa huyo na kufikiria uamuzi huo wa kumfungulia mlango wa kutokea.

Manchester, England. Manchester United imekubali kumtoa kwa mkopo kipa Andre Onana kwenda Trabzonspor baada ya kukosa imani na mkali huyo wa Cameroon.

Baada ya kushuhudia makosa inaeleweka wazi kwanini Man United imechoshwa na kipa huyo na kufikiria uamuzi huo wa kumfungulia mlango wa kutokea.

Onana ameshindwa kufanya vizuri Old Trafford tangu alipotua akitokea Inter Milan 2023, ambapo kiwango chake kizuri kimezidiwa na matukio ya kuboronga ndani ya uwanja.

Haya hapa makosa yake 22 ambayo yalichangia moja kwa moja Man United kufungwa mabao katika miaka yake miwili ya kipa huyo aliyokuwa golini.

22. v Arsenal (Septemba 2023)

Declan Rice alipiga mpira kwenye msitu wa mabeki wa Man United na kumbabatiza mmoja wa mabeki hao. Onana aliruka bila ya mafanikio akiishia kuugusa mpira kwa mkono mmoja, angeweza kufanya vizuri.


21. v Brentford (Oktoba 2023)

Kipa Onana alionekana kama ameshadaka shuti la Mathias Jensen na mpira huo ukionekana kupungua kazi, lakini kitu cha ajabu ulimtoka na kuingia kwenye nyavu za Man United.


20. v Bournemouth (Aprili 2024)

Justin Kluivert aliingia ndani ya boksi la Man United na kumpiga shuti hafifu kwenye nguzo ya karibu aliyokuwa Onana, lakini kipa huyo hakuwa amefanya kitu chochote mpira ukitinga nyavuni.


19. v Bodo/Glimt (Novemba 2024)

Philip Zinckernagel alipiga mpira kupita kwenye uvungu wa miguu ya kipa Onana wakati kipa huyo alipojaribu kubana miguu yake mpira usipite na kutinga kwenye nyavu za Man United.


18. v Galatasaray (Novemba 2023)

Onana alishindwa kabisa kudaka mpira wa adhabu uliopigwa na Hakim Ziyech kutoka nje ya boksi na mpira huo uliingia nyavuni wakati kipa huyo wa Man United akiungalia tu.

ONA 01

17. v Nottingham Forest (Desemba 2024)

Onana alishindwa kuruka kudaka mpira wa kichwa wa Chris Wood, ambapo mpira huo ulimvuka, ukagonga mwaba na kutinga nyavuni kuifanya Man United kuruhusu bao jingine la uzembe wa kipa.


16. v Copenhagen (Novemba 2023)

Onana aliukamata mpira kwa mikono yake miwili baada ya shuti la Lukas Lerager, lakini cha ajabu mpira huo ulimponyoka na kutinga nyavuni na kuiweka Man United kwenye nyakati ngumu katika  Ligi ya Mabingwa.

ONA 02

15. v West Ham (Desemba 2023)

Kabla ya Krismasi kwenye mechi huko West Ham, staa Jarrod Bowen aligonga mpira kuusukumia nyavuni baada ya kipa Onana kushindwa kuokoa mpira na kumwangushia mfungaji miguuni.


14. v Aston Villa (Desemba 2023)

John McGinn alifunga kwa mkwaju wa adhabu, ambapo mpira uliopita ukuta wa Man United ulimpita Onana juu ya kichwa chake bila kufanya chochote kuzuia shuti hilo lisitinge nyavuni.


13. v Grimsby (Agosti 2025)

Staa wa Grimsby, Charles Vernam alipiga shuti kutoka upande wa kushoto wa Man United na wakati huo Onana hakuwa na kizuizi chochote cha kuona mpira, lakini ulimponyoka na kutinga kwenye nyavu.

12. v Tottenham (Mei 2025)

Hili lilitokea kwenye mechi ya fainali ya Europa Leaguem anbapo Onana alishindwa kufanya vizuri na kumruhusu Brennan Johnson kufunga bao pekee kwenye mechi hiyo na kuipa Tottenham ubingwa.


11. v Ipswich (Februari 2025)

Onana na Patrick Dorgu walishindwa kuwasiliana vyema kuhusu mpira uliokuwa unaelekea ndani ya boksi na wakati kipa huyo akitoka langoni, Dorgu alipiga mpira na Jaden Philogene kufunga kirahisi.

ONA 03

10. v Man City (Mei 2024)

Wakati Man United ikiwabana majirani zao kwenye fainali ya Kombe la FA, Jeremy Doku alipiga mpira akiwa nje ya boksi na kipa Onana aliishia kuutazama tu mpira huo ukivuka mstari wa goli lake.


9. v Nottingham Forest (Desemba 2024)

Morgan Gibbs-White alipiga mpira katikati ya goli la Man United na mpira huo ulimvuka kipa Onana, akifungwa kizembe kabisa na kuwachefua mashabiki wa Man United.


8. v Galatasaray (Novemba 2023)

Mabao mawili ya mikwaju ya adhabu ya Ziyech kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya huko Uturuki, ilidhihirisha ubovu wa Onana kwenye goli la Man United na kuigharimu pakubwa timu hiyo kwenye michuano ya Ulaya.


7. v Grimsby (Agosti 2025)

Onana alitoka golini kwake baada ya mpira kupigwa ndani ya boksi, alipojaribu kumpiga ngumi mpira badala ya kuudaka na kuufanya kuangukia karibu na goli lake kuwapa Grimsby urahisi wa kufunga.


6. v Viktoria Plzen (Desemba 2024)

Onana alijaribu kumpigia pasi mchezaji mwenzake kabla ya kuguswa na Pavel Sulc, aliyekimbilia ndani ya boksi na kumpigia pasi Matej Vydra, aliyesukumua mpira nyavuni akiwa mbele ya nyavu tupu.

ONA 05

5. v Bayern Munich (Septemba 2023)

Leroy Sane alipiga shuti akiwa nje ya boksi na Onana alijaribu kuruka kuokoa mpira huo kitu cha ajabu ulimpira na ukatinga nyavuni. Hiyo ilikuwa mechi yake ya kwanza ya Ulaya akiwa na Man United.


4. v Galatasaray (Oktoba 2023)

Wakati Man United ikipambana dhidi ya Galatasaray huko Old Trafford, Onana alimpasia mpira mguuni mpinzani Dries Mertens na kusababisha Casemiro kutolewa kwa kadi nyekundu alipojaribu kuokoa jahazi.


3. v Lyon (Aprili 2025)

Onana alishindwa kuzuia shuti kwenye dakika 95 katika robo fainali ya Europa League na mchezaji Rayan Cherki alifurahia hilo baada ya kuwahi mpira huo na kuifungia timu yake bao la kusawazisha.

ONA 04

2. v Lyon (Aprili 2025)

Mapema kwenye mechi ya Lyon, Onana alishuhudia shuti la mbali la Thiago Almada likitinga kwenye nyavu zake na yeye akiwa amesimama tu bila ya kufanya hiyo na kuonyesha siku mbaya kwa kipa huyo katika mechi hiyo.


1. v Nottingham Forest (Agosti 2023)

Wakati Taiwo Awoniyi akiingia kwenye goli la Man United, kipa Onana alianguka kitako wakati alikuwa akijaribu kupambana na jambo hilo lilimfanya kunyanyuka kwa wakati na mpira ukitinga nyavuni.