Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Manchester United yaongeza dau kwa Mbeumo

Muktasari:

  • Mbeumo alifunga mabao 20 kwenye Ligi Kuu England msimu uliopita.

Manchester, England. Manchester United wameongeza rasmi ofa yao kwa mshambuliaji wa Brentford, Bryan Mbeumo, hadi kufikia Pauni milioni 70 (Sh245 bilioni) katika juhudi mpya za kumaliza mkwamo uliodumu kwa wiki kadhaa kwenye mazungumzo ya usajili wake.

Awali, United walitoa ofa ya pauni milioni 62.5, sawa na kiasi walichotumia kumsajili Matheus Cunha kutoka Wolves, lakini ofa hiyo ilikataliwa na Brentford. Sasa, kwa kulenga kumaliza dili hilo, United wamewasilisha dau jipya la pauni milioni 65, likiwa na nyongeza ya pauni milioni 5.

Mbeumo, ambaye amekuwa wazi kutaka kujiunga na United, atasubiri klabu hizo mbili zikubaliane ili apate kufanyiwa vipimo vya afya. Hii ina maana kuwa huenda asiwepo kwenye kikosi kitakachocheza mechi ya kirafiki dhidi ya Leeds United huko Stockholm, Sweden Jumamosi, lakini anaweza kujumuishwa katika msafara wa ziara ya Marekani wiki ijayo.

Endapo usajili huo utakamilika, Mbeumo atakuwa mchezaji wa tatu kusajiliwa na United katika dirisha hili la majira ya joto, akifuata nyayo za Matheus Cunha na beki chipukizi Diego Leon.

Kocha mkuu Ruben Amorim atakuwa ametimiza azma yake ya kusajili wachezaji wawili wa nafasi ya namba 10 kwa mfumo wake wa 3-4-2-1, akitumia jumla ya zaidi ya pauni milioni 130 (Sh455 bilioni) kwa Cunha na Mbeumo.

Mbeumo, mwenye umri wa miaka 25, alifunga mabao 20 kwenye Ligi Kuu England msimu uliopita na pia amezivutia klabu kama Arsenal, Newcastle United, na Tottenham, inayofundishwa na aliyekuwa kocha wake Brentford, Thomas Frank.

United walihitaji mshambuliaji wa aina yake baada ya kuonyesha udhaifu mkubwa wa kutupia wavuni msimu uliopita ambapo walifunga jumla ya mabao 44 pekee, ikiwa ni takwimu ya pili mbaya zaidi kwa timu isiyoshuka daraja tangu kuanzishwa kwa EPL mwaka 1992.

Mbeumo ameibuka kuwa mshambuliaji hatari tangu ajiunge na Brentford mwaka 2019 kwa ada ya pauni milioni 5.8, akifunga mabao 70 katika mechi 242, ikiwa ni pamoja na mabao 42 kwenye mechi 136 za EPL.

Mafanikio haya yamepatikana chini ya uongozi wa Thomas Frank, ambaye hivi karibuni aliteuliwa kuwa kocha mpya wa Tottenham baada ya kuiongoza Brentford kwa miaka saba.

Wakati huo huo, beki wa zamani wa United Rio Ferdinand amewatahadharisha Mashetani Wekundu dhidi ya kusuasua kwenye dili hilo:

“United inapaswa kumalizana na Brentford sasa. Dili hili limekuwa kwenye vyombo vya habari kwa muda mrefu sana. Wakiingia dirisha linafungwa bila kumchukua Mbeumo, hiyo itakuwa aibu kubwa.

“Mbeumo anafaa kimwili, ana kasi, anafunga mabao EPL, na anaijua ligi. Nafikiri anaendana na mahitaji ya United kwa sasa,” amesema kupitia kipindi chake cha Rio Ferdinand Presents.