Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mazungumzo ya Simba, FCC yamkuna Waziri Bashungwa

Muktasari:

  • Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, Innocent Bashungwa ameipongeza Tume ya Ushindani nchini (FCC) na klabu ya Simba kwa kumaliza mgogoro wao.

Dar es Salaam. Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, Innocent Bashungwa ameipongeza Tume ya Ushindani nchini (FCC) na klabu ya Simba kwa kumaliza mgogoro wao.

Amezitaka klabu nyingine za soka nchini kuiga mfano huo ili kuleta maendeleo ya mchezo wa mpira wa miguu.

Ijumaa Aprili 16, 2021 akiwa bungeni jijini Dodoma,  Bashungwa alizungumzia mgogoro huo wa vikwazo vilivyoibuka katika mchakato wa mabadiliko ya uendeshaji wa klabu ya Simba na kusema huenda ukamalizika Jumatatu Aprili 19, 2021 wakati FCC itakapokutana kwa mara ya tatu na pande zinazohusika.

Kabla ya Bashungwa kutoa kauli hiyo bungeni, Jumanne Aprili 13, 2021 mwenyekiti wa bodi ya Wakurugenzi ya Simba, Mohammed Dewji 'Mo' kupitia mtandao wake wa kijamii wa Twitter

Mazungumzo ya Simba, FCC yamkuna Waziri Bashungwa

alieleza kusikitishwa kwake na FCC akidai kuwa uongozi wa klabu hiyo na FCC wanafanya vikao na baada ya kumaliza wanaandikiwa barua ya kuwataka waanze upya mchakato.

Lakini leo Jumamosi Aprili 24, 2021 kupitia ukurasa wa mtandao wa kijamii wa Instagram wa Wizara ya Habari, Bashungwa ametoa pongezi alipotembelea mradi wa ujenzi wa kituo cha michezo cha Shirikisho la Soka nchini

(TFF) kilichopo Kigamboni, Dar es Salaam.

"Nazikaribisha klabu nyingine kushirikiana na Serikali ili kuendana na dira ya Serikali na maelekezo ya Rais wetu Samia Suluhu Hassan ya kutaka sekta hii kutoa ajira kubwa sana kwa vijana na kuchangia kwenye pato la nchi," amesema Waziri Bashungwa.

Bashungwa ametumia nafasi hiyo pia kuipongeza Simba kwa kufika hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika, huku akiwasihi Watanzania kuonyesha uzalendo wa kuiunga mkono timu hiyo inayoitangaza nchi ya Tanzania kimataifa na kupitia kauli mbiu ya timu hiyo ya ‘Visit Tanzania’.

Simba kwa sasa inasubiri kujua itapangwa na timu gani katika droo itakayofanyika Aprili 30, jijini Cairo, Misri lakini timu za CR Belouizdad na MC Alger za Algeria pamoja na Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini mojawapo ina nafasi kubwa ya kukutana na vinara hao wa Ligi Kuu Bara kwa sasa.