Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mbappe atambulisha saa mpya Ligi ya Mabingwa Ulaya bei yake yatajwa

Muktasari:

  • Staa huyo wa Real Madrid ameungana na wabunifu wa saa kali duniani, Hublot kutengeneza saa hiyo mpya iliyotengenezwa kwa nakshi za Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Madrid, Hispania. Supastaa, Kylian Mbappe ametambulisha saa mpya ya Ligi ya Mabingwa Ulaya. Staa huyo wa Real Madrid ni barozi wa wabunifu wa saa kali duniani, Hublot ambao wamebuni saa hiyo mpya iliyotengenezwa kwa nakshi za Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Mbappe, 26, amecheza mechi 87 kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya na kufunga mabao 55. Hata hivyo, bado hajabeba taji hilo na matarajio yake ni ya kulibeba baada ya kujiunga na miamba hiyo ya La Liga yenye maskani yake Bernabeu.

Hublot ndio wadhamini wakuu wa saa kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya tangu 2015.

Kampuni hiyo imetengeneza saa maalumu zaidi ya 800 na nembo yake imekuwa ikionekana kwenye kibao cha kubadilisha wachezaji na kuonyesha muda wa mechi kinachotumika na mwamuzi wa akiba kwenye mechi.

Na sasa imeamua kutengeneza saa itakayokuwa maalumu kwa michuano hiyo ya Ligi ya Mabingwa Ulaya. Toleo jipya la saa hizo, ambazo zitakuwa chache sana na zitauzwa kwa Pauni 11,800 zaidi ya Sh40 milioni za Kitanzania.

Saa hizo zina mikanda ya mpira ya rangi nyeusi na bluu na imewekwa logo ya Mabingwa Ulaya. Mbappe ndiye aliyetumika kwenye utambulisho wa saa hizo kwa ajili ya msimu huu.

Kwa mteja atakayeamua kutoa karibu Pauni 12,000 kununua saa hiyo, atapewa pia kikombe kidogo cha Ligi ya Mabingwa Ulaya kama zawadi.

Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Hublot, Julien Tornare alisema: "Soka si tu ni mchezo ni hisia. Kuanzia kwenye kelele za mashabiki hadi kwenye ukimya wa kupigiana penalti, kila pigo lina hisia. Hii saa imetengenezwa kwa hisia hiyo. Hilo ndilo lililotusukuma, kwa sababu hatupimi muda, tunausherehekea."

Mbappe si mwanasoka mwenyewe aliyeamua kuingia kwenye dunia ya utengenezaji wa saa, akiwamo Cristiano Ronaldo, ambaye amekuwa na saa zake mwenyewe nembo ya Jacob & Co, ambazo bei yake inaanzia Pauni 22,000 hadi Pauni 92,000 ambazo ni pesa za Kitanzania zaidi ya Sh73.7 milioni hadi Sh308 milioni mtawalia.