Mwesigwa aahidi uwazi, Dalali, Mtawala, Dauda waula TFF

Katibu mkuu mpya wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Selestine Mwesigwa.PICHA|MAKTABA
Muktasari:
Mwesigwa aliwahi kuwa Kkatibu Mmkuu wa Yanga kabla ya kuvunja mkataba na klabu 2012
Dar es Salaam. Katibu mkuu mpya wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Selestine Mwesigwa ametambulishwa rasmi jana kuchukua mikoba ya Angetile Osiah na kuahidi kufanya kazi kwa uwazi na ushirikiano.Akizungumza mara baada ya kutambulishwa na Rais wa TFF, Jamal Malinzi, Mwesigwa alisema, “Nnitatumia uzoefu
wangu na elimu yangu kuhakikisha naifanya kazi yangu kwa weledi, nitalinda masilahi ya shirikisho, nitakuwa muwazi, nitatoa ushirikiano kwa kila mtu na kupokea mawazo ya watu, yale nitakayoona yana manufaa nitayachukua na kuyafanyia kazi kwa masilahi ya shirikisho.“Milango ipo wazi na ikibidi kukosolewa nikosolewe pale itakapoonekana inafaa, kikubwa naomba ushirikiano kwa watu wote, vyama vya mikoa, klabu, vyama shiriki na wadau wote wa soka.” alisema Mwesigwa ambaye alikingiwa kifua na Rais Malinzi pale alipoulizwa ana jipya gani TFF wakati alishakuwa katibu ya Yanga na akatimuliwa kwa kile kilichoelezwa ni utendaji mbovu.
Hata hivyo swali hilo lilizimwa na Malinzi ambaye alisema kwa kifupi “Yaliyopita Yanga yamepita, kilichotokea Yanga tulifuatilia na kujua ni kwa nini walimtoa, tumemuona Mwesigwa ni mtu safi, ana rekodi nzuri tusiangalie ya nyuma, tuanzia hapa tulipo tusonge mbele.” alisema Malinzi.Pia alimtangaza Katibu wa Simba, Evodius Mtawala kuwa mMkurugenzi wa vyama wanachama na masuala ya kisheria nafasi ambayo ilikuwa wazi baada ya Mtemi Ramadhani kumaliza muda wake kipindi cha uongozi uliopita.Mbali na kumtangaza Mwesigwa na Mtawala, pia Malinzi alisitisha ajira ya Saad Kawemba aliyekuwa Mkurugenzi wa Mashindano nafasi ambayo anaitumikia hadi Desemba 31 mkataba wake utakapomalizika.Malinzi alisema nafasi hiyo ilipaa waombaji kadhaa kutoka ndani na nje ya TFF, lakini waombaji wote hawakupewa nafasi hiyo na kamati ya utendaji imeagiza nafasi hiyo itangazwe upya na wale wote walioomba mara ya kwanza wasiombe tena na oafisa itifaki wa TFF, Idd Mshangama atakaimu nafasi hiyo.
“Pia nafasi ya mkurugenzi wa ufundi imebaki wazi baada ya waombaji wote kutokidhi vigezo hivyo itatangazwa upya, Salum Madadi ambaye ni afisa mashindano wa TFF atakaimu nafasi hiyo, hali kadhalika kwa nafasi ya Mkurugenzi wa Fedha na Utawala nafasi ambayo pia imebaki wazi itakaimiwa na Danny Msangi.Awali Seleki Yonaza alikuwa akikaimu nafasi hiyo na waombaji walioomba awali hawaruhusiwi kuomba tena.”alisisitiza Bonifance Wambura ambaye alikuwa akikaimu katibu mkuu amerudi kwenye wadhifa wake wa ofisa habari wa TFF.
Malinzi alisema kuwa ajira hizo zitaanza rasmi Januari Mosi mwaka 2014.Wakati huo huo Kamati hiyo ya utendaji imepitisha kamati ya uchaguzi na kamati ya rufaa ambazo zitaongozwa na mawakili ile ya uchaguzi itaongozwa na Wakili Melchesedck Lutema akisaidiwa na Walter Chipeta, Hamidu Omar, Jeremiah Wambura na Hassan Dalali wakati Kamati ya Rufaa ya uchaguzi itaongozwa na Julius Lugaziya, Mwita Waisaka, Juma Khamis, Rashid Dilunga na Masoud Issangu.Mbali na Kamati hizo za uchaguzi pia imeteua kamati ndogo inayohusika na mpira wa ufukweni ‘Beach Soccer’ ambayo itaongozwa na Mwenyekiti wa Ashanti United ambaye pia ni mjumbe wa kamati ya utendaji kupitia mkoa wa Kigoma/Tabora, Ahmed Mgoyi akisaidiwa na Shafii Dauda, Deo Lucas, Juma Mgunda, Bonifance Pawasa, Joseph Kanakamfumu na John Mwansasu.