Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Nabi amuita Mayele Kaizer Chiefs

Mshambuliaji Fiston Mayele akiwa na Kocha Nabi enzi wakiwa Yanga. Picha na Maktaba

Muktasari:

  • Mtandao wa Kingfut wa Misri umefichua kuwa miongoni mwa mapendekezo ya mwanzo ambayo Nabi ameupa uongozi wake muda mfupi baada ya kujiunga na timu hiyo ni kuhakikisha Mayele anaichezea timu hiyo msimu ujao.

Afrika Kusini. Kocha mpya wa Kaizer Chiefs, Nasreddine Nabi ameuomba uongozi wake kuhakikisha unamsajili mshambuliaji wa Pyramids FC, Fiston Mayele kwa ajili ya kuimarisha safu yao ya ushambuliaji.

Mtandao wa Kingfut wa Misri umefichua kuwa miongoni mwa mapendekezo ya mwanzo ambayo Nabi ameupa uongozi wake muda mfupi baada ya kujiunga na timu hiyo ni kuhakikisha Mayele anaichezea timu hiyo msimu ujao.

Kiwango bora ambacho Mayele anakionyesha kwenye Ligi Kuu ya Misri lakini pia ufahamu ambao Nabi anao kwa Mayele kutokana na kuwahi kufanya naye kazi walipokuwa Yanga zinaonekana kuwa sababu ambazo zimemfanya kocha huyo atamani kufanya tena kazi na mshambuliaji huyo raia wa DR Congo.

Mayele amekuwa moto wa kuotea mbali katika Ligi Kuu ya Misri msimu huu ambapo hadi sasa anaongoza chati ya kufumania nyavu akiwa amefunga mabao 14.

Lakini pia mshambuliaji huyo amepiga pasi tano za mwisho na hivyo kuchangia kuifanya timu yake kuongoza msimamo wa ligi kuu ya Misri.

Hata hivyo kikwazo kwa Kaizer Chiefs kinaonekana kitakuwa ni fedha ambazo Pyramids itahitaji ili kumuachia mshambuliaji huyo.

Ikumbukwe Mayele alinunuliwa na klabu hiyo ya Misri mwaka jana kwa dau la Dola 800,000.