Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Namna Salah alivyoishawishi Liverpool kumsajili Frimpong

Muktasari:

  • Mohamed Salah amemaliza msimu wa 2024/2025 akiwa mfungaji bora wa Ligi Kuu England (EPL), akiwa amepachika mabao 29.

Muda mfupi baada ya Liverpool kukamilisha usajili wa beki wa kulia Jeremie Frimpong kutoka Bayer Leverkusen, sababu za kiufundi zinazomhusisha mshambuliaji Mohamed Salah zimeonekana kushawishi uhamisho huo.

Uwezo wa kushambulia kwa kupunguza mabeki ambao Frimpong mwenye umri wa miaka 24 anao, unategemewa kuwa chachu ya kuongeza namba ya magoli ya Salah kwa vile inaonekana ujio wa beki huyo mpya utawafanya walinzi wa timu pinzani kuachia mianya ambayo nyota huyo wa Misri anaweza kuipata baada ya kazi itakayokuwa ikifanywa na Frimpong.

Inaaminika kuwa Liverpool inataka kumpunguzia Salah eneo kubwa la kukimbia kwa kumsajili Frimpong ikiamini kuwa umri wa miaka 33 ambao mfungaji huyo bora wa EPL msimu uliomalizika anao, utamfanya asiwe na kasi kubwa kulinganisha na hapo nyuma.

Lakini pia Frimpong anayemudu pia kucheza eneo la juu kama winga, anategemewa kuziba nafasi ya Salah pindi staa huyo wa Misri atakapoondoka klabuni hapo kwenda kuitumikia timu yake ya taifa katika Fainali za Mataifa ya Afrika (AFCON) 2025 mwishoni mwa mwaka huu.

Ukiondoa hizo, sababu nyingine inayoonekana imeishawishi Liverpool kumsajili Jeremie Frimpong ni historia nzuri ya beki huyo kutopata majeraha ya mara kwa mara au ya muda mrefu.

Hilo limemfanya Frimpong kucheza idadi kubwa ya mechi na kuwa mchezaji tegemeo wa Bayer Leverkusen hadi pale timu hiyo ya Ujerumani ilipoamua kumuuza.

Katika misimu miwili iliyopita, Frimpong amecheza idadi ya mechi 95 kati ya 103 ya Leverkusen ambapo amekosekana katika michezo nane tu.

Liverpool imemsajili Frimpong  ili awe mbadala wa Trent Alexander-Arnord ambaye ameachana na timu hiyo kwa ajili ya kujiunga na Real Madrid ambayo ilikuwa ikimuwania kwa muda mrefu.

Uhamisho wa Jeremie Frimpong umeigharimu Liverpool kiasi cha Pauni 29.5 milioni (Sh107 bilioni) ambapo mchezaji huyo atatumikia kikosi cha mabingwa hao wa EPL 2025 kwa mkataba wa miaka mitano.