Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ofa zamfuata Casemiro akiaga Man United

Muktasari:

  • Casemiro alijiunga na Manchester United mwaka 2022 akitokea Real Madrid kwa uhamisho uliogharimu Pauni 60 milioni (Sh204 bilioni).

Ofa mbalimbali zimeanza kumiminika kwa kiungo wa Manchester United, Casemiro baada ya mchezaji huyo raia wa Brazil kutangaza hatoitumikia timu hiyo msimu ujao.

Miongoni mwa ofa hizo, zimetoka kwa klabu ya LA Galaxy inayoshiriki katika Ligi Kuu ya Marekani (MLS).

Wakati mashabiki wengi wa klabu hiyo wakitamani aongeze mkataba, mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 33 amesema kuwa ataondoka klabuni hapo.

“Nitaibeba Manchester United siku zote za maisha yangu. Kuanzia siku ya kwanza nilipotembea katika uwanja huu mzuri, nilihisi hamasa ya Old Trafford na upendo ambao sasa ninashirikiana na mashabiki wa klabu hii ya kipekee.

“Sio muda wa kusema kwaheri. Kuna kumbukumbu nyingi za kutengeneza katika miezi minne ijayo. Tuna mengi ya kupigania pamoja. Shabaha yangu kamili itabakia siku zote kutoa kila kilicho changu kuisaidia klabu hii ifanikiwe,” amesema Casemiro.

Inaripotiwa kwamba miongoni mwa ofa nono ambazo ziko mezani mwa Casemiro ni ya LA Galaxy ambayo inataka kumsajili kiungo huyo kwa mkakati maalum.

Galaxy inaamini kumsajili Casemiro kutasaidia kuongeza mvuto wa Marekani katika kuandaa Fainali za Kombe la Dunia 2026.

Ofa nyingine zinatoka Saudi Arabia na pia zipo timu za kwao Brazil ambazo zinamhitaji.