Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ronaldo na mkataba wa kufuru Al Nassr

Muktasari:

  • Mkataba huyo mpya ambao Ronaldo ameandaliwa unaonekana kuwa ni matunda ya uongozi mpya wa Al Nassr ambao umeteuliwa hivi karibuni.

Riyadh, Saudi Arabia. Al Nassr imeamua kuonyesha jeuri ya pesa ili kumshawishi nyota wake Cristiano Ronaldo kusaini mkataba mpya wa kuendelea kuitumikia timu hiyo ya Saudi Arabia.

Klabu hiyo imepanga kufanya mambo mawili ambayo hapana shaka yatamshawishi Ronaldo kuendelea kuitumikia Al Nassr kwa kuongeza mkataba mpya wa mwaka mmoja baada ya huu wa sasa kufikia tamati, Juni mwaka huu.

Katika mkataba huo mpya, Ronaldo atapokea kitita cha Pauni 167.9 milioni (Sh519 bilioni) kwa mwaka ambao utamfanya nyota huyo mwenye umri wa miaka 39 kuwa mwanamichezo anayelipwa zaidi duniani.

Lakini kana kwamba haitoshi, Al Nassr itampa Ronaldo kiasi cha Pauni 49 milioni (Sh152 bilioni) kutokana na shughuli za nje ya uwanja ambazo itamtumia au kutumia picha zake.

Ikiwa Ronaldo atasaini mkataba huo, maana yake atalipwa kiasi cha Pauni 3.19 milioni kwa wiki sawa na Shilingi 9.9 bilioni kwa wiki na kwa siku atapata kitita cha Pauni 419,000 (Sh1.3 bilioni).

Ukizigawa fedha hizo kwa dakika, maana yake katika kila dakika, Ronaldo atapata kitita cha Pauni 291 (Sh 899787).

Ukiondoa kipengele hicho cha fedha, Al Nassr pia atapewa haki ya kumiliki asilimia tano za hisa za klabu hiyo.

Mkataba huyo mpya ambao Ronaldo ameandaliwa unaonekana kuwa ni matunda ya uongozi mpya wa Al Nassr ambao umeteuliwa hivi karibuni.

Ronaldo aliyejiunga na Al Nassr mwaka 2023, amekuwa mchezaji tegemeo wa timu hiyo ambapo katika mechi 84 alizoichezea, ameifungia mabao 75.