Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Roy Keane auona mwisho wa England Kombe la Dunia

Muktasari:

  • England itashuka tena dimbani Julai 5 mwaka huu kuvaana na wenyeji wenza Mexico katika mchezo wa kuwania tiketi ya kwenda hatua ya robo fainali.

Nahodha wa zamani wa Manchester United na timu ya taifa ya Ireland, Roy Keane, amesema anaamini safari ya England katika Fainali za Kombe la Dunia 2026 itaishia hatua ya robo fainali, akidai timu hiyo haina uwezo wa kuongeza kiwango chake dhidi ya mataifa makubwa.

Kauli hiyo imekuja baada ya England kutoka nyuma na kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya DR Congo katika hatua ya 32 bora, ushindi uliopatikana kupitia mabao mawili ya nahodha Harry Kane ndani ya dakika 15 za mwisho.

Ushindi huo umeifanya England kutinga hatua ya 16 bora, ambapo itakutana na Mexico katika Uwanja wa Azteca, Mexico City.

Akizungumzia mechi inayofuata kwa timu hiyo, Keane amesema anaamini England inaweza kuiondoa Mexico kutokana na ubora wa wachezaji kama Harry Kane na Jude Bellingham, lakini akaonya kuwa changamoto kubwa itaanza iwapo itakutana na Brazil au Argentina.

"Nilipoitazama England dhidi ya DR Congo nilijua mwisho watashinda kwa sababu wana mchezaji kama Harry Kane ambaye anaweza kukuokoa wakati mgumu.

"Nafikiri wataifunga Mexico, lakini wakikutana na Brazil au Argentina ndipo matatizo yataanza. Wakicheza kama walivyocheza dhidi ya DR Congo, watatolewa," amesema Keane.

Keane amesisitiza kuwa England imefikia kiwango chake cha juu na haina uwezo mkubwa wa kubadilisha mchezo inapokutana na wapinzani wenye ubora mkubwa.

"Sidhani kama England ina kiwango kingine cha ziada cha kuonyesha. Wana wachezaji wachache wa kiwango cha dunia ambao wanaweza kubadili matokeo, lakini hilo lina mipaka yake.

“Ndiyo maana ninaamini wataishia robo fainali. Ukiangalia timu kama Ufaransa, bado wana asilimia 20 zaidi ya kiwango cha kuonyesha," ameongeza.

Mbali na hilo, Keane amemkosoa kipa wa England, Jordan Pickford kufuatia bao la mapema lililofungwa na Brian Cipenga wa DR Congo.

Kwa maoni yake, Pickford alipaswa kuokoa mpira huo baada ya kuugusa kwa mkono.

"Kinachonitia wasiwasi ni kipa. Kama ana kiwango cha juu, angejilaumu mwenyewe kwa bao lile. Siamini hoja kwamba makipa hawapaswi kufungwa kwenye nguzo ya karibu kila wakati, lakini kama umeugusa mpira kwa mkono, unapaswa kuuzuia," amesema.

England itashuka tena dimbani Julai 5 mwaka huu kuvaana na wenyeji wenza Mexico katika mchezo wa kukata tiketi ya kwenda hatua ya robo fainali.