Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Hizi hapa sababu refa Msomalia kuzuiwa Marekani

Muktasari:

  • Kuzuiliwa kwa Artan kuingia Marekani kumezima ndoto yake ya kuandika historia ya kuwa refa wa kwanza wa Somalia kuchezesha Fainali za Kombe la Dunia.

New York, Marekani. Msemaji wa Idara ya Forodha na Ulinzi wa Mipaka ya Marekani (CBP), amethibitisha kuwa mwamuzi wa Somalia, Omar Abdulkadir Artan, alizuiwa kuingia nchini humo kutokana na wasiwasi unaohusiana na masuala ya usalama.

Mnamo Juni 6, Artan aliwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Miami akitokea Uwanja wa Ndege wa Istanbul.

Wakati wa mchakato wa kuingia Marekani, refa huyo alifanyiwa ukaguzi wa ziada, ambao ni utaratibu wa kawaida unaotumiwa na idara hiyo pale maafisa wanapohitaji kuthibitisha taarifa au kubaini kama mtu anaruhusiwa kuingia nchini.

Baada ya ukaguzi kukamilika, ilibainika kuwa msafiri huyo, ambaye ni mwamuzi wa Kombe la Dunia, hakuruhusiwa kuingia Marekani kutokana na masuala ya uhakiki wa usalama, hivyo akanyimwa ruhusa ya kuingia nchini humo.

"Wasafiri wote wanaotaka kuingia Marekani, wakiwemo wanamichezo, makocha na maafisa wa kiufundi, hufanyiwa ukaguzi na uchunguzi na Idara ya Forodha na Ulinzi wa Mipaka.

"Maamuzi ya kuruhusu au kutoruhusu mtu kuingia nchini hufanywa kwa kuzingatia kila kesi kivyake, kwa kutumia taarifa zilizopo kutoka vyombo vya sheria, usalama wa taifa na uhamiaji wakati wa ukaguzi.

"Maafisa wa CBP pia wana mamlaka ya kuwahoji wasafiri, kufanya upekuzi na kuamua iwapo mtu apewe au anyimwe ruhusa ya kuingia nchini kwa mujibu wa sheria za Marekani," imesema taarifa ya CBP.

Kuzuiliwa kwa Artan kuingia Marekani kumezima ndoto yake ya kuandika historia ya kuwa refa wa kwanza wa Somalia kuchezesha Fainali za Kombe la Dunia.

Mwaka 2025, Artan alitangazwa kuwa Refa Bora Afrika kwa Wanaume na msimu huu amechezesha mechi ya pili ya fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.