Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Sababu Ubelgiji kutopewa penalti dhidi ya Hispania

Muktasari:

  • Katika mchezo huo ulichezwa kwenye Uwanja wa SoFi, Calfornia, Hispania ilishinda kwa mabao 2-1, mabao ya Hispania yakiwa yamepachikwa na Fabian Luiz na Mikel Merino huku lile la Ubelgiji likipachikwa na Charles De Ketelaere.

Katika mchezo dhidi ya Hispania Jana, Ijumaa, Julai 10, 2026, Refa Michael Oliver aliibua mjadala baada ya kuamua kutoipa penalti Ubelgiji katika dakika ya 61, kutokana na kitendo cha kiungo Rodri kugusa kwa mkono mpira katika eneo la hatari la Hispania.

Mpira huo ulikuwa umeokolewa na beki Aymeric Laporte na ukatua kwa Rodri ambaye alijikuta akinawa lakini Refa Oliver hakuamua kuipa tuta Ubelgiji.

Hata hivyo kwa tafsiri ya sheria ya 12 ya soka inayohusu faulo na utovu wa nidhamu, Rodri alinusurika kwa vile tukio alilofanya linahesabika kama mpira ulifuata mkono.

Sheria za hiyo inaeleza wazi kwamba si kosa la mpira wa mkono pale mpira unapogonga mkono wa mchezaji moja kwa moja baada ya kuchezwa kutoka kichwani au mwilini mwa mchezaji mwenzake aliyekuwa karibu, kiasi kwamba mchezaji huyo hana nafasi halisi ya kuitikia au kujiepusha.

Katika tukio hilo, mpira ulitoka kwa beki wa Hispania aliyekuwa karibu sana na kisha ukaugonga mkono wa mchezaji mwenzake. Hivyo, hilo si kosa la mkono kufuata mpira.

Sababu nyingine muhimu zilizounga mkono uamuzi wa mwamuzi ni mpira ulitoka umbali mfupi sana na huyo hakuwa na muda wa kuukwepa mpira kugonga mkono wake.

Katika mchezo huo ulichezwa kwenye Uwanja wa SoFi, Calfornia, Hispania ilishinda kwa mabao 2-1, mabao ya Hispania yakiwa yamepachikwa na Fabian Luiz na Mikel Merino huku lile la Ubelgiji likipachikwa na Charles De Ketelaere.

Hispania ndio ilikuwa ya kwanza kupata bao kupitia kwa Luiz katika dakika ya 30 baada ya kumalizia mpira uliiokolewa na safu ya ulinzi ya Ubelgiji.

Hata hivyo Ubelgiji ilisawazisha katika dakika ya 41 kupitia Ketelaere aliyefunga kwa kuunganisha kwa kichwa krosi ya Timothy Castagne.