Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Salah mlangoni Saudia

Muktasari:

  • Slot amekiri kuwa hajui kama Salah bado ataendelea kuwepo katika kikosi chake msimu ujao.

Riyadh, Saudia Arabia. Ofisa Mtendaji Mkuu wa Ligi Kuu Saudi Arabia amethibitishwa rasmi kwamba mshambuliaji wa Liverpool, Mohamed Salah ni miongoni mwa wachezaji wanaohitaji kuwa nao katika ligi yao kwa dirisha lijalo la majira ya baridi.

Bosi huyo wa Ligi ya Saudia, Omar Mugharbel amesema wao kama viongozi wa ligi wangependa kuona Salah akisajiliwa na moja ya timu zao.

Nyota huyo wa Liverpool, aliachwa nje ya kikosi kilichocheza mechi ya ushindia wa 1-0 katika Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Inter Milan, juzi Jumanne kutokana na kiwango kisichoridhisha alichokuwa anakionyesha tangu kuanza kwa msimu huu, pia maeneno yake ya hivi karibuni yaliyoonekana kumkera kocha Arne Slot.

Salah mwenye umri wa miaka 33, alisema anaona Liverpool ni kama inamwondoa na kujaribu kumfanya mbuzi wa kafara kwa kumwangushia jumba bovu juu ya matokeo ya timu.

Licha ya kuwindwa na klabu za Saudi katika dirisha lililopita la majira ya kiangazi, staa huyo raia wa Misri alisaini mkataba mpya wa kuendelea kusalia katika kikosi hicho hadi mwaka 2027.

Akizungumza na waandishi wa habari katika tamasha la World Football Summit, Mugharbel amesema: "Salah anakaribishwa kwenye Ligi ya Saudi, lakini majukumu ya mazungumzo juu ya maslahi na mambo mengine yapo kwa klabu. Bila shaka, Salah ni mmoja wa wachezaji wanaohitajika na timu hizo."

Salah mwenye umri wa miaka 33, haonekani kuwa na uwezekano wa kuendelea kusalia Liverpool kutokana na kile kinachoendelea baina yake na benchi la ufundi.

Kocha Arne Slot amesema hajamjuisha tena Salah katika kikosi chake kutokana na maneno aliyoyatoa dhidi yake pamoja na timu kwa ujumla.

Salah ambaye pia alithibitisha kwamba uhusiano wake na kocha Slot umevunjika  aliweka wazi pia kuwa haoni kama ataendelea kubakia katika kikosi cha majogoo hao na mechi ijayo dhidi ya Brighton inaweza kuwa ya mwisho kwake kucheza au kuonekana kwani baada ya hapo atasafiri kwenda kuungana na kikosi cha timu ya taifa ya Misri kwa ajili ya kucheza mechi za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON).

Haijulikani kama atacheza mechi hiyo, hasa baada ya kuposti picha zake za mazoezini akiwa peke yake wakati wachezaji wenzake wakiwa wamesafiri kwenda Italia wiki hii.

Mwaka 2023, Al-Ittihad iliwasilisha ofa ya takribani Pauni 150 milioni ili kumpata Salah, lakini ilikataliwa na sasa tovuti ya The Sun imefichua kwamba Al-Hilal inafikiria kumsajili.

Slot amekiri kuwa hajui kama Salah bado ataendelea kuwepo katika kikosi chake msimu ujao.