Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Saliba aiingiza sokoni Arsenal ikimfuata Konsa

Muktasari:

  • Saliba alipata maumivu ya mgongo katika mchezo wa nusu fainali ya Kombe la Dunia dhidi ya Hispania, yaliyomlazimisha afanyiwe mabadiliko katika dakika ya 20 na kuingia Maxence Lacroix.

Maumivu ya mgongo ambayo William Saliba ameyapata katika Fainali za Kombe la Dunia 2026, yameilazimisha Arsenal kuingia sokoni kusaka beki wa kati na inamuona Ezri Konsa wa Aston Villa kama mbadala sahihi.

Saliba alipata maumivu hayo yaliyomlazimu afanyiwe mabadiliko katika dakika ya 30 ya mchezo kwa kuingia Maxence Lacroix huku timu yake Ufaransa ikimaliza kwa kufungwa mabao 2-0.

Inaripotiwa kwamba Saliba anaweza kuwa nje ya uwanja kwa muda wa miezi minne hadi mitano jambo ambalo limeifanya Arsenal isake beki mpya.

Na Konsa ambaye kwa sasa yupo na kikosi cha England katika fainali za Kombe la Dunia anaonekana kuwa kipaumbele cha Meneja wa Arsenal, Mikel Arteta.

Konsa ambaye mkataba wake wa sasa na Aston Villa umebakiza muda wa miaka miwili, ameonekana kusuasua kusaini mkataba mpya ambao utamfanya aendelee kuitumikia klabu yake kwa muda mrefu zaidi na jambo hilo linaipa nguvu Arsenal ikiamini inaweza kumnasa kirahisi.

Kingine kinachoipa imani Arsenal kwamba inaweza kumpa Konsa ni changamoto ya kifedha ambayo inaikabili Aston Villa iliyochangiwa na klabu hiyo kuvuka kiwango cha matumizi hivyo kulazimika kwanza kuuza wachezaji ili ipate fursa ya kununua wapya.

Ulazima huo wa kuuza wachezaji ndio umeifanya Aston Villa iwaruhusu Youri Tielemans kwenda Manchester United na Lucas Digne kujiunga na PSG.

Konsa amekuwa miongoni mwa wachezaji wanaotajwa kuwa mabeki bora wa kati katika Ligi Kuu England.