Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Senegal yasalia kileleni kundi D

Muktasari:

  • Congo inasalia na pointi moja pekee na itakamilisha mechi zake za makundi dhidi ya Nigeria.

Mabingwa watetezi, Senegal wameendelea kuongoza kundi D la mashindano ya Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani (CHAN 2024) licha ya kutoka sare ya bao 1-1 dhidi ya Congo katika mechi ya pili wa kundi hilo iliyochezwa leo, Agosti 12, 2025, kwenye Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar.

Sare hiyo imeipa pointi moja muhimu na kuimarisha nafasi yake ya kufuzu hatua ya robo fainali ya michuano hiyo ambayo inafanyika kwa mara ya nane.

Congo ndiyo walikuwa wa kwanza kupata bao dakika ya 19, baada ya mshambuliaji Dechan Moussavou kumalizia pasi ya Atipo.

Senegal ilijitahidi kusawazisha kipindi cha kwanza kwa kushambulia mara kwa mara, lakini ilikumbana na ukuta mgumu wa Congo.

Kipindi cha pili kilianza kwa mabadiliko makubwa upande wa Senegal, ambapo kocha aliingiza wachezaji wapya akiwemo Vieux Cisse, Ousseynou Seck na Fonseca.

Lengo lilikuwa kuongeza kasi na ubunifu katika safu ya ushambuliaji, jambo lililoongeza presha kwa Congo.

Jitihada hizo zililipa dakika ya 82 baada ya Seck kutoa pasi  iliyomkuta Samb  ambaye alimalizia na kuisawazishia Senegal.

Kwa matokeo haya, Senegal inafikisha pointi nne na kuendelea kushika nafasi ya kwanza kwenye Kundi D, ikifuatiwa na Sudan yenye pointi moja ambayo itashuka dimbani baadaye leo kumenyana na Nigeria.

Congo inasalia na pointi moja pekee na itakamilisha mechi zake za makundi dhidi ya Nigeria.