Simba wafuzu hatua ya makundi kibabe

Wednesday January 06 2021
simba pic
By Ramadhan Elias

MCHEZO wa Klabu Bingwa Afrika kati ya Simba na FC Platinum umemalizika kwa Simba kuibuka na Ushindi wa bao 4-0, mabao yaliyofungwa na Erasto Nyoni, Shomari Kapombe, John Bocco na Clatous Chama.

Kipindi cha pili kilianza kwa Simba kuendelea walipoishia kwani waliingia kwa kushambulia kama ilivyokuwa kipindi cha kwanza na dakika ya 50, Luis Miqquisone alipiga mkwaju wa faulo uliogonga mwamba wa juu baada ya kuangushwa na beki wa Platinum nje kidogo ya boksi la 18.

Fc Platinum nao walionekana kuchachamaa kwa kwani katikati ya dakika 50 hadi 55 waliweza kupata kona mbili ambazo hazikuleta  madhara yeyote kwenye lango la Simba, pia dakika ya 57 mshambuliaji mmoja wa Platinum alikosa bao la wazi akiwa amebaki yeye na kipa na kupiga mpira uliotoka nje.

Dakika ya 60 Simba walifanya mabadiliko kwa kumtoa Said Ndemla na nafasi yake kuchukuliwa na Ibrahim Amme na dakika ya 61 Simba wakapata bao la pili kupitia kwa beki wao wa kulia Shomari Kapombe.

Baada ya bao hilo la pili kwa Simba mchezo  mchezo kwa ujumla ulifunguka na timu zote mbili kuanza kucheza kws kutafuta bao japo Plutinum walionekana kuliandama mara kwa mara goli la Simba.

Dakika ya 75 Simba walifanya mabadiliko mengine kwa kwa kumtoa Straika Chriss Mugalu na nafasi yake kuchukuliwa na Meddie Kagere.

Advertisement

Dakika 85 John Bocco aliingia kwa upande wa Simba kuchukua nafasi ya Meddie Kagere aliyeumia dakika chache baada ya kuingia kuchukua nafasi ya Chriss Mugalu.

Dakika ya 90 John Bocco aliiandikia Simba bao la tatu na la mwisho kwa mchezo huo baada ya kumalizia pasi safi ya Rally Bwalya.

Dakika ya 90 (Nyongeza) Simba walipata bao la nne kupitia Chama kwa mkwaju wa Penalti baada ya Chama huyo huyo kuangushwa ndani ya boksi la 18 na mlinzi mmoja wa Platnum.

Ushindi  huo wa bao 4-0 unawafanya Simba kufuzu hatua ya Makundi ya michuano hiyo kwa jumla ya bao 4-1, kutokana na mchezo wa kwanza uliochezwa Zimbabwe FC Platinum kushinda kwa bao moja pekee.

Advertisement