Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Simba, Yanga Oktoba 20

mashabiki wa timu ya Yanga ya jijini Dar es salaam, wakishangilia katika moja ya mechi za ligi kuu ya Vodacom dhidi ya watani wao wa jadi Simba

Muktasari:

Pia, mahasimu hao wanatarajiwa kuufunga mzunguko wa pili Aprili 27 mwakani wakati watakapocheza mechi ya marudiano kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Dar es Salaam. Mahasimu wa kihistoria wa Soka la Tanzania, Simba na Yanga wataumana Oktoba 20 katika mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu Tanzania Bara katika pambano litakalopigwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Pia, mahasimu hao wanatarajiwa kuufunga mzunguko wa pili Aprili 27 mwakani wakati watakapocheza mechi ya marudiano kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), mwenyeji wa mechi ya kwanza atakuwa Simba wakati mechi ya marudiano mwenyeji atakuwa Yanga.

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa TFF, Angetile Osiah alisema Ligi Kuu ya Tanzania Bara itaanza rasmi Agosti 24 na kumalizika Aprili 27, 2014.

Osiah alisema pambano la kufungua msimu (Ngao ya Jamii) kati ya bingwa mtetezi Yanga na mshindi wa pili msimu uliopita, Azam litakalopigwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam Agosti 17.

Alisema, mzunguko wa kwanza wa ligi hiyo utamalizika Novemba 3 mwaka huu wakati wa pili utamalizika Aprili 27 mwakani

Osiah, pia alizitaka klabu shiriki zihakikishe zinamiliki viwanja vyao vya mazoezi sambamba na kuwasilisha TFF taarifa za ukaguzi wa hesabu kabla ya msimu mpya kuanza.

“Soka letu haliwezi kupiga hatua kama klabu kila siku zinahangaika kutafuta sehemu za kufanyia mazoezi, bado tunalisisitiza suala hilo, klabu zinatakiwa ziwe na viwanja zinavyovimiliki, pia zihakikishe zinakabidhi ripoti za ukaguzi wa fedha kabla ya ligi kuanza,” alisema Osiah.

Kwa mujibu wa ratiba hiyo mabingwa watetezi Yanga wataanza kutetea taji lao kwa kuwakaribisha Ashanti United kwa mara nyingine katika Ligi Kuu (Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam).

Watani zao Simba wenyewe wataanzia ugenini Tabora wakiwa wageni wa timu ngeni iliyopanda Ligi Kuu kwa mara ya kwanza Rhino Rangers kwenye Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi, Tabora.

Mabingwa 1999, Mtibwa Sugar wenyewe watakuwa wenyeji wa Azam (Uwanja wa Manungu, Morogoro), huku Mbeya City wakianza ligi hiyo nyumbani kwa kuivaa Kagera Sugar (Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine, Mbeya).

Michezo mingine ni Mgambo Shooting na JKT Ruvu (Uwanja wa Mkwakwani, Tanga), JKT Oljoro na Coastal Union (Uwanja wa Sheikh Kaluta Amri Abeid, Arusha), Ruvu Shooting na Tanzania Prisons (Uwanja wa Mabatini, Mlandizi, Pwani).