Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Singida Black Stars yataka ubingwa Kagame Cup ikianza na Wahabeshi

Muktasari:

  • Mashindano ya Kombe la Kagame 2025 yanashirikisha idadi ya timu 12 kutoka nchi wanachama wa Baraza la Vyama vya Mpira wa Miguu Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) na nyingine zilizoalikwa.

Wakati Singida Black Stars ikirusha kete yake ya kwanza leo kwenye mashindano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati (Kombe la Kagame), benchi la ufundi na wachezaji wa timu hiyo wametamba kuwa wanataka kubakisha ubingwa nyumbani.

Timu hiyo leo Jumatatu, Septemba 2, 2025 itakabiliana na Coffee ya Ethiopia katika Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo, Dar es Salaam ukiwa ni mchezo wa kundi A.

Kocha Mkuu wa Singida Black Stars, Miguel Gamondi amesema kuwa siku zotte amekuwa akipenda timu anayofundisha ifanye vizuri hivyo anaingia katika Kombe la Kagame akiwaza ubingwa na sio kushiriki tu.


"Ni mashindano mazuri kutathmini wachezaji wetu ukizingatia sasa tuna wachezaji watatu hadi wanne katika timu za taifa hii inatupa uwezekano wa kuwapa nafasi wachezaji wengine. Kucheza mechi za kirafiki sio sawa na kucheza mechi za mashindano kama hizi ambazo mnakuwa na mashabiki na timu nzuri kutoka nje.

"Nadhani ni nzuri kwetu na tunachukua haya kama sehemu ya maandalizi lakini mimi ni mshindani na tunataka kushindana na tupo hapa kushindana na lengo letu ni kushinda. 

Kwangu mimi mpira wa miguu ni kitu cha kufanya watu wapate burudani hivyo nawasisitiza wachezaji wangu kuhakikisha tunapata ushindi na tunacheza vizuri," amesema Gamondi.

Beki mpya wa Singida Black Stars, Nickson Kibabage amesema kuwa wachezaji wa timu hiyo wapo tayari kwa mashindano hayo.

"Kikubwa tumejiandaa vizuri na mashindano haya na tunayachukulia kama maandalizi kwa ajili ya mashindano ya kimataifa. Kwa hiyo tuna imani maandalizi yameenda vizuri na tunawaomba mashabiki waendelea kutupa sapoti timu yao ili tuweze kufanya vizuri," amesema Kibabage.

Hii ni mara ya pili kwa Singida Black Stars kushiriki mashindano ya Kombe la Kagame ambapo mara ya kwanza ilikuwa ni mwaka jana ilipoishia hatua ya makundi.

Timu hiyo ilimaliza ikiwa katika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa kundi C ambalo ilikuwa imepangwa na timu za SC Villa ya Uganda, APR ya Rwanda na Al-Merreikh Bentiu ya Sudan Kusini.

Ilipata ushindi katika mchezo mmoja dhidi ya Bentiu ambao ilishinda kwa mabao 3-1 lakini ilipoteza kwa bao 1-0 dhidi ya APR na ikafungwa mabao 3-1 na SC Villa.

Msimu huu Singida Black Stars itaiwakilisha Tanzania Bara katika mashindano ya Kombe la Shirikisho Afrika ambayo katika hatua ya awali imepangwa kukutana na Rayon ya Rwanda.

Mchezo wa kwanza itakuwa ugenini Rwanda ambao umepangwa kuchezwa kati ya Septemba 19 hadi 21 mwaka huu na timu hizo zitarudiana nchini Tanzania kati ya Septemba 26 hadi 28, 2025.

Mshindi wa mechi mbili baina ya Singida Black Stars na Rayon Sports, atakutana na mshindi wa michezo miwili itakayozikutanisha Flambeau du Centre ya Burundi na Al Akhdar ya Libya.