Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Singida BS yalazimishwa sare Kagame na wapinzani pungufu

Muktasari:

  • Hii ni Mara ya pili kwa Singida Black Stars kushiriki Kombe la Kagame ambapo mara ya kwanza ilikuwa ni mwaka jana ilipoishia hatua ya makundi.

Singida Black Stars imeanza kwa matokeo ya sare tasa kwenye mashindano ya Kombe la Kagame dhidi ya Ethiopian Coffee kwenye Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo.

Katika mechi hiyo ya kwanza ya kimashindano kwa kocha huyo wa zamani wa Yanga, Miguel Gamondi tangu alipopewa mikoba ya kuongoza kikosi hicho, Singida BS ilionekana kutokuwa na makali katika safu yake ya ushambuliaji.

Ndani ya dakika 45 za kipindi cha kwanza, Singida BS  ilitengeneza nafasi tatu za wazi huku ikionekana kumtumia zaidi Andrew Phiri ambaye alikuwa akishambulia kutokea pembeni, hata hivyo ilishindwa kuzitumia.

Ethiopian Coffee iliwabidi kucheza pungufu kwa zaidi ya dakika 30 katika kipindi cha pili kufuatia kipa wao, Ibrahim Danland kuonyeshwa kadi nyekundu.

Kipa huyo alionyeshwa kadi hiyo moja kwa moja kutokana na kudaka mpira akiwa nje ya eneo lake, hivyo aliadhibiwa huku Singida BS ikipewa faulo ambayo iliipotea.

Licha ya Gamondi kufanya mabadiliko kadhaa kwenye safu yake ya ushambuliaji ikiwemo kuingia kwa Elvis Rupia, Ethiopian Coffee ilikuwa imara kutokana na idadi kubwa ya wachezaji ambayo ilikuwa nyuma hasa baada ya kuwa pungufu.

Ibrahim amekuwa mchezaji wa kwanza kuonyeshwa kadi nyekundu katika mashindano haya ya Kombe la Kagame.

Katika mchezo ujao Singida BS itacheza dhidi ya Polisi ya Kenya ambayo imeanza mashindano hayo kwa kishindo kufuatia kuichapa  Garde-Cotes ya Djibouti  mabao 4-0.