Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Slot ataka ushindi Ulaya kuituliza Liverpool

Kocha wa Liverpool, Arne Slot wakati akihojiwa na wanahabari kabla ya mtanange dhidi ya Galatasaray katika Ligi ya Mabingwa Ulaya. Picha na Mtandao

Muktasari:

  • Mshindi wa jumla wa mchezo baina ya Liverpool na Galatasaray atakutana na PSG ambayo tayari imetinga hatua ya robo fainali kwa kuitupa nje Chelsea.

London, England. Meneja wa Liverpool, Arne Slot, amekiri kuwa amefanya makosa kadhaa msimu huu kufuatia matokeo yasiyoridhisha ya timu hiyo, lakini anaamini ushindi katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Galatasaray leo Jumatano, Machi 18, 2026 unaweza kubadili taswira hasi iliyopo kwa sasa.

Liverpool wanakabiliwa na presha kubwa baada ya kupoteza kwa bao 1-0 katika mchezo wa kwanza uliochezwa jijini Istanbul, matokeo yanayowalazimu kushinda kwa tofauti ya mabao mawili ili kufuzu hatua ya robo fainali ya michuano hiyo.

Akizungumzia hali ya mashabiki kuonyesha kutoridhishwa, Slot amesema iwapo kweli mashabiki hawafurahii mwenendo wake, basi ni ishara kuwa kuna mambo mengi hayajaenda sawa chini ya uongozi wake.

“Nilielezwa nilipokuja hapa kuwa klabu hii ina utamaduni wa kumuunga mkono kocha kwa muda mrefu. Kama kweli mashabiki hawafurahii, basi ina maana nimefanya makosa mengi, na hilo si jambo la kufurahisha,” amesema Slot.

Hata hivyo, kocha huyo raia wa Uholanzi amesisitiza kuwa ushindi unaweza kubadilisha hali ya mambo haraka katika soka, akieleza kuwa kikosi chake kiko tayari kwa mchezo huo muhimu.

Katika Ligi Kuu England, Liverpool wamekuwa na msimu mgumu na matumaini yao makubwa kwa sasa ni kumaliza ndani ya nafasi tano za juu, huku pia wakitegemea kufanya vizuri kwenye mashindano mengine ili kurejesha imani ya mashabiki.

Kwa upande wake, nahodha msaidizi Andy Robertson amesema anaelewa hasira za mashabiki baada ya matokeo mabaya ya hivi karibuni, akisisitiza kuwa jukumu la wachezaji ni kuhakikisha wanawarejeshea furaha.

“Lengo letu siku zote ni kuwaacha mashabiki wakiwa na furaha wanapoondoka Anfield. Mara hii hawakuwa na furaha, na tunaelewa hilo,” amesema Robertson.

Ameongeza kuwa mazingira ya Anfield wakati wa mechi za usiku mara nyingi huleta matokeo ya kipekee, na ana matumaini kuwa hali hiyo itajirudia dhidi ya Galatasaray.

Katika taarifa nyingine ya kikosi, Liverpool wanakabiliwa na changamoto ya majeraha kutoka kwa beki, Joe Gomez huku Ibrahima Konate akitarajiwa kurejea baada ya kupona tatizo dogo la misuli.

Kocha Slot pia amesema mshambuliaji Alexander Isak anaendelea kuimarika na yupo karibu kurejea mazoezini na wenzake, ingawa bado anahitaji muda zaidi kabla ya kurejea uwanjani rasmi.

Mshindi katika mchezo huo atakutana na PSG ambayo tayari imetinga hatua ya robo fainali baada ya kuitupa nje Chelsea.