Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ethiopia, Taifa Stars kukipiga Dar

Muktasari:

“Mashindano yalikuwa mazuri, tulienda na nia ya kurudi na kombe, lakini hatujafanya hivyo ila muhimu ni kwamba mashindano haya yametupa uzoefu mkubwa ili tuweze kujiandaa na mashindano mengine ambayo yako mbele yetu,” alisema Kim.

TIMU ya taifa ya Ethiopia inatarajia kucheza mechi za kirafiki za kimataifa na Tanzania pamoja na Morocco kwa ajili ya kujiandaa na Fainali za Mataifa ya Afrika 2013.

Taarifa zinasema Ethiopia itakabiriana na Tanzania jijini Dar es Salaam kabla ya kuivaa Morocco Januari 12, huko Johannesburg.

Chanzo cha habari kutoka mjini Addis Ababa kinasema bado tarehe ya mechi ya Tanzania haijapangwa ila inatarajiwa kuchezwa mwezi Januari kabla ya kuanza kwa Fainali za Mataifa ya Afrika.

"Ethiopia itacheza mechi za kimataifa za kirafiki dhidi ya Tanzania na Morocco kwa ajili ya kujiandaa na fainali za Afrika,"kilisema chanzo kimoja cha habari mjini Ethiopia.

Akizungumzia ratiba hiyo Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Angetile Osiah alisema wao bado hawajapata taarifa juu ya mechi hiyo.

"Taarifa kuhusu mchezo huo bado hazijanifikia na hatujui lolote," alijibu Osiah kwa kifupi.

Tayari Tanzania na Morocco zimethibitisha kucheza mechi za kirafiki za kimataifa na mabingwa wa Afrika Zambia, mechi zitakazochezwa mjini Dar-es-Salaam na Johannesburg.

Tanzania itacheza na Zambia Desemba 22 mjini Dar es Salaam wakati Morocco itacheza na Zambia mjini Johannesburg Januari 8.

Ethiopia na Zambia ambazo zipo kundi katika makundi ya timu zitakazoshiriki Fainali za Mataifa ya Afrika 2013, zote zitapata mechi za kujipima nguvu dhidi ya Tanzania.

Ethiopia na Zambia zipo Kundi C pamoja na timu za Nigeria na Burkina Faso, ambapo zitakuwa zikicheza mechi zao za hatua ya makundi kwenye uwanja wa Mbombela huko Nelspruit, Afrika Kusini mwakani kwani fainali hizo za Afrika zinatarajiwa kuanza Januari 19 na kumalizika Februari 10.

Wakati huohuo; Kocha Kim Poulsen leo anategemea kutangaza kikosi kitakachoingia kambini kujiandaa na mchezo dhidi ya Zambia hapo Desemba 23.

Kim aliyeiongoza timu ya Tanzania Bara 'Kilimanjaro Stars' katika  michuano ya Kombe la Chalenji amerejea jana nchini pamoja na timu hiyo.

Akizungumza baada ya kurejea, kocha Kim alisema mashindano yalikuwa muhimu sana kwa timu yake kwani vijana wamepata uzoefu baada ya kukutana na timu ngumu na zenye uzoefu.

“Mashindano yalikuwa mazuri, tulienda na nia ya kurudi na kombe, lakini hatujafanya hivyo ila muhimu ni kwamba mashindano haya yametupa uzoefu mkubwa ili tuweze kujiandaa na mashindano mengine ambayo yako mbele yetu,” alisema Kim.

Alisema,“tumefarajika kucheza na timu kubwa kama Uganda ambayo ndiyo timu bora katika Ukanda wa Afrika ya Mashariki na Kati.” .

Kim alisema sasa hivi macho ya wachezaji wake wote yako katika mchezo ujao wa kirafiki dhidi ya Zambia 'Chipolopolo' kwani ni mechi ambayo itakuwa kipimo kikubwa kwa Stars kwa hivyo inahitaji maandalizi makubwa sana.

“Nawaomba Watanzania wasikate tamaa kwa kuwa tunaijenga timu,  hawa ni vijana na ninaamini siku zijazo watafanya vizuri zaidi,” alisema Kim.