Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Yondani, Domayo waikosa Stars

Yondani

Muktasari:

Katika hatua nyingine, Domayo na Yondani juzi jioni walikwama mjini Istanbul baada ya tiketi zao walizotumiwa kujiunga na Stars iliyoko kambini Ethiopia kutowaruhusu kwani zinaonyesha wanatakiwa kwenda Februari 9, wakati Stars tayari ipo Addis Ababa.

KIUNGO Frank Domayo na beki Kelvin Yondani wameshindwa kujiunga na Taifa Stars kutokana na utata wa tiketi zao na leo wataichezea Yanga katika mchezo wake wa mwisho wa kirafiki dhidi ya Emmen ya Uholanzi kwenye Uwanja wa Adora.

Emmen inashiriki Ligi Daraja la Kwanza Uholanzi, ambapo jana kocha mkuu wa timu hiyo, Joop Gal alithibitisha kwenye mtandao wa klabu hiyo kwamba watacheza na Yanga na itakuwa ni kipimo kizuri kwao katika kambi ya mazoezi mjini hapa, pia tayari timu ya FC Ordabasy ya Kazakhstan anayochezea Mganda Andy Mwesigwa imetua Uturuki kwa ajili ya kuweka kambi.

Mechi ya leo itakuwa ya tatu na mwisho kwa Yanga hapa Uturuki baada ya kucheza na Arminia Buelefeld ya Ujerumani na kutoka sare ya bao 1-1 kabla ya kufungwa na Denizlispor mabao 2-1.
Mchezo huo wa leo wa Yanga utapigwa kwenye Uwanja wa Adora football ulioko kilomita 55 kutoka ilipo kambi ya Yanga, ambapo kwa usafiri wa Taxi ni zaidi ya Sh200,000 kwenda na kurudi mji wa Antalya.

Yanga ambayo ipo mjini hapa kwa wiki ya pili sasa, kocha wake Ernest Brandts amesema mechi hii ni kipimo kizuri kwa kuwa timu wanayocheza nayo ina mseto wa wachezaji mbalimbali wa kimataifa ambao wamekuwa na ushindani mkubwa kwenye ligi za Uholanzi.

Katika hatua nyingine, Domayo na Yondani juzi jioni walikwama mjini Istanbul baada ya tiketi zao walizotumiwa kujiunga na Stars iliyoko kambini Ethiopia kutowaruhusu kwani zinaonyesha wanatakiwa kwenda Februari 9, wakati Stars tayari ipo Addis Ababa.

Baada ya kushindikana kurudisha nyuma tiketi hizo wachezaji hao walilazimika kurudi kambini mjini Antalya kuendelea na mazoezi na wenzao. Kutoka Antalya mpaka Instanbul kwa ndege ni muda wa dakika 50.

Akizungumzia sakata hilo la wachezaji hao kushindwa kujiunga na Stars, Katibu mkuu wa TFF, Angetile Osiah alikiri kuwapo kwa makosa ya tarehe hizo. “Ni kweli tumegundua tiketi tulizozituma kulikuwa na makosa ya tarehe badala ya kuandikwa Januari 9 zikaandikwa Februari 9, ni makosa yaliyofanywa na wakala wa shirika la ndege,” alisema Osiah.

Alisema, “Kwanza tulitaka Domayo na Yondani wapande ndege ya kupitia Entebe na kuja Dar es Salaam, tukaambiwa na wakala kuwa ndege imejaa hivyo tukawaomba watupangie ile inayopitia Addis Ababa kwa tarehe 9 mwezi huu, lakini wale mawakala walifanya makosa kuandika mwezi wa pili.”

Yanga itamaliza kambi yake ya mazoezi mjini hapa Jumamosi, ambapo Jumapili mchana itaanza safari ya kurejea Dar es Salaam na itawasili Jumatatu saa 10 alfajiri. Timu kutoka Mataifa mbalimbali ya Ulaya zipo mjini Antalya, Uturuki kwa ajili ya kambi za mazoezi kujianda na ligi za nchi zao, Yanga ikiwa ndiyo timu pekee kutoka Afrika hadi sasa.

Hata hivyo, mjini Antalya kuna wachezaji wengi wanaozurura mjini kutoka Afrika ya Kati na Magharibi wakitafuta timu za kufanya majaribio.