Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Tanzania Prisons yaipeleka Yanga Tabora ikiomba radhi mashabiki

Muktasari:

  • Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya ulifungiwa jana, Jumatatu, Machi 7, 2026 kwa kukosa vigezo vya kikanuni na sheria za mpira wa miguu. 

Siku moja baada ya shirikisho la soka Tanzania (TFF) kuufungia uwanja wa Sokoine jijini Mbeya kwa kukosa sifa ya kuchezewa mechi za mashindano, Tanzania Prisons imehamishia mchezo wake dhidi ya Yanga katika Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora.

Sokoine ulifungiwa jana Machi 8, 2026 ikiwa ni saa chache baada ya mchezo wa Kombe la Shirikisho la CRDB baina ya Mbeya City dhidi ya Bandari FC ulioisha kwa wenyeji kushinda mabao 3-0 na kufuzu 16 bora.

Wakati Uwanja huo ukifungiwa Prisons ilikuwa ikijiandaa kuikaribisha Yanga katika mchezo wa kiporo katika mwendelezo wa Ligi Kuu, Machi 12 mwaka huku Mbeya City ikijinoa kuwapokea Singida Black Stars, Machi 15.

Akizungumza na Mwananchi leo Machi 9, 2026, Afisa Mtendaji Mkuu wa Tanzania Prisons, Ajabu Kifukwe amewaomba radhi mashabiki na wadau wa soka jijini Mbeya kwa kuhamisha mechi hiyo akieleza kuwa ni jambo lililo nje ya uwezo wao.

Amesema uongozi unaomba radhi pia kwa matokeo yasiyoridhisha akieleza kuwa kwa sasa wachezaji wana ari na nguvu mpya tangu walipomaliza mchezo wao dhidi ya Azam FC ulioisha kwa suluhu ya bila kufungana akieleza kuwa matarajio yao ni kufanya vizuri.

"Mchezo wetu dhidi ya Yanga utachezwa Tabora katika Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi. Tumejipanga kushinda baada ya kutokuwa na mwanzo mzuri, ari ya wachezaji iko juu na tunaomba radhi kwa mabadiliko haya yaliyonje ya uwezo wetu.

"Kuhusu hamasa nje ya Uwanja, hii ni timu ya Taasisi na imekuwa na utaratibu wake pale inaposhinda huwa Mkuu wa Jeshi la Magereza huwa anatoa ofa, hii ni mwendelezo, tunaenda kwa kujiamini kutafuta pointi tatu,” amesema Kifukwe.

Ameongeza kuwa benchi la ufundi chini ya kocha Shedrack Nsajigwa limekuwa na program nzuri na wachezaji wakijiandaa na mchezo huo muhimu akiahidi kuwa Prisons inahitaji ushindi ili kujiweka pazuri katika msimamo wa Ligi Kuu.

Hadi sasa Tanzania Prisons wamecheza mechi 15 na kuvuna pointi 13 na kuwa nafasi ya 15, huku Yanga wakiwa kileleni kwa pointi 32 kwa mechi 12 huku ikiwa imefunga mabao 28.

Hata hivyo wakati timu hizo zikienda kukutana, Yanga imeonekana kuwa na rekodi bora dhidi ya Maafande hao, kwani mara ya mwisho Prisons kushinda mbele ya bingwa huyo mtetezi ilikiwa Mei 10, 2018 ilipoilaza mabao 2-0.