Tchakei kumrithi Chama Simba
Muktasari:
- Klabu ya Simba imewasilisha ofa kwa Singida ikihitaji saini Tchakei ambaye anatajwa kuja kuchukua nafasi ya Chama.
Dar es Salaam. Simba imewasilisha ofa kubwa kwa Singida Fountain Gate wakitaka huduma ya kiungo wao mshambuliaji Marouf Tchakei.
Simba inamtaka Tchakei akachukue nafasi ya kiungo Clatous Chama ambaye ambaye mkataba wake unafikia ukingoni mwisho wa msimu.
Hata hivyo Singida bado haijafanya uamuzi wa mwisho kutokana na mezani kuna ofa kubwa zaidi kutoka Ihefu ya Mbeya.
Ihefu imefika mbali kutaka huduma ya Tchakei baada ya timu hiyo kununuliwa na kigogo mmoja mzito.
Simba inaona Tchakei ni chaguo sahihi kwao kuja kuziba nafasi ya Chama ambaye kocha Abdelhak Benchikha hataki kuendelea naye endapo atapata mrithi wake.
Bado hakuna uhakika wa dili hilo mpaka sasa wakati muda ukizidi kuyoyoma kabla ya kufungwa kwa dirisha la usajili saa 6:00 usiku leo.