Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ten Hag hatamani tena ukocha

Muktasari:

  • Katika maisha ya ukocha, Erik Ten Hag amezinoa Manchester United, Ajax, FC Utrecht,  Go Ahead Eagles na PSV Eindhoven.

Meneja wa zamani wa Manchester United, Erik Ten Hag amesema kuwa anaweza kutokuwa na mpango wa kurejea katika kazi hiyo kutokana na ugumu aliokumbana nao miaka ya hivi karibuni.

Ten Hag alifukuzwa kazi na Manchester United mwanzoni mwa msimu huu kutokana na mwenendo usioridhisha wa timu hiyo na nafasi yake kuchukuliwa na Ruben Amorim.

Katika kipindi cha miaka miwili na ushee ambayo Ten Hag ameitumikia Manchester United, timu hiyo ilifanikiwa kutwaa mataji mawili ambayo ni Kombe la FA na Kombe la Carabao.

Tangu alipoachana na Manchester United, Ten Hag hajapata timu nyingine ya kuinoa na kocha huyo amefichua kwamba hadhani kwamba anaweza kuwa na mawazo kama mbele ya safari atarudia kusimamia timu.

"Kuna mambo mengi ninaweza kufanya. Labda kwenye mpira wa miguu kwa nafasi nyingine kama ya umeneja hiyo ni chaguo. Na labda kitu cha tofauti kabisa," amesema Ten Hag.

Inaripotiwa kwamba Ten Hag ana mpango wa kutumia muda mwingi kushughulikia usimamizi wa mradi wa usimamizi wa majengo ambao umeifanya familia yake kuwa miongoni mwa familia tajiri huko Uholanzi.

Na hilo limethibitishwa na Ten Hag mwenyewe ambapo amefichua kuwa ni jambo analolihusudu kando ya mpira wa miguu.

"Lakini tunaendesha pamoja na baba yangu tunaendesha kampuni. Hicho ni kitu kingine ambacho napenda kukifanya. Kwa sasa ninaweza kukipa uangalizi mkubwa na kinavutia," amesema Ten Hag.

Ten Hag amesema sababu ambayo inamfanya afikirie kutojihusisha tena na ukocha ni ugumu wa kuwafundisha wachezaji wa kizazi cha sasa.

Kutimuliwa kwa Ten Hag kulikuja baada ya Manchester United kupata ushindi katika mechi tatu tu kati ya tisa za mwanzo kwenye EPL msimu huu.

Hata hivyo bado mambo yanaonekana kuiendea kombo Man United chini ya Amorim ambapo kwa sasa timu hiyo inashika nafasi ya 15 katika msimamo wa Ligi Kuu England (EPL).