Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

TFF kujadili tamko la Serikali

Muktasari:

“Waziri ametimiza wajibu wake kwa mujibu wa mamlaka zinazompa uwezo wa kuingilia kati inapoonekana kuna tatizo,” alisema Rage.

SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF), limeitisha kikao cha dharura Kamati ya Utendaji ili kujadili tamko la Wizara ya Habari, Vijana Utamaduni na Michezo kutokuitambua katiba ya sasa ya shirikisho hilo.

Waziri mwenye dhamana ya michezo, Fenella Mukangara juzi alieleza msimamo wa Serikali kutokuitambua katiba hiyo iliyotumika kwenye mchakato wa Uchaguzi Mkuu wa TFF na badala yake wanaitambua ile ya mwaka 2006.

Mwaka jana, TFF ilipitisha waraka kwa wajumbe wake kwa ajili ya mabadiliko ya katiba ili kutimiza matakwa ya Fifa na Shirikisho la Soka Afrika (CAF), ambapo asilimia 70 ya wajumbe walikubali mapendekezo yaliyoleta katiba mpya ya TFF.

Mukangara alisema katiba mpya ya TFF haitambuliki na Serikali kwa vile imekiuka kanuni ya Baraza la Michezo Tanzania (BMT) namba 11, ibara ya kwanza.

Ofisa Habari wa TFF, Boniface Wambura alisema wamepata barua kutoka serikalini kutengua uamuzi wa msajili wa Klabu na Vyama vya Michezo kuidhinisha marekebisho ya Katiba ya TFF toleo la 2012.

Alisema baada ya kupokea barua hiyo, Sekretarieti iliwasiliana na Rais wa TFF, Leodegar Tenga ambaye ameagiza kuitishwa kwa  kikao cha dharura Jumamosi.

Akizungumzia uamuzi huo, Mwenyekiti wa Simba, Ismail Aden Rage alisema kwa vile Serikali haitambui katiba ya sasa ya TFF, ingekuwa busara kwa shirikisho hilo kufuta Ligi Kuu.

Rage alisema hana tatizo na uamuzi wa wizara kwani ndiyo yenye jukumu la kusimamia michezo nchini na kupitisha katiba ya chama chochote.

“Waziri ametimiza wajibu wake kwa mujibu wa mamlaka zinazompa uwezo wa kuingilia kati inapoonekana kuna tatizo,” alisema Rage.

Rage alisema hatua ya wizara kutokutambua katiba ya TFF ambao ni wasimamizi wa mchezo wa soka, maana yeke ligi pia imepoteza heshima hivyo ifutwe. “Sisemi hivyo kwa sababu Simba sasa ipo katika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi, ila ni kuangalia ukweli wa jambo lenyewe.”

Aliongeza kuwa ligi hii inaendeshwa kwa kanuni za katiba mpya 2013, na kama Serikali wameifuta basi moja kwa moja na mashindano yanapaswa kufutwa pia.

Katibu Mkuu wa TFF, Angetile Osiah alisema kama waziri haitambui katiba ya sasa, basi hata Ligi Kuu haitambuliki, mashindano ya kimataifa yanayozishirikisha Simba na Azam pia hayatambuliki kwani katiba iliyotumika ni ya mwaka 2012.

“Tumefanya mabadiliko mengi tangu 2006 mpaka kufikia jana. Ina maana mabadiliko yote hayatambui?” alihoji Osiah.

Aliongeza: “Mikoa ya Katavi, Geita, Simiyu inatambulika kwa sasa kama mikoa wanachama wapya TFF kupitia mabadiliko ya katiba hiyo, nayo ifutwe kwa sababu tu katiba iliyotumika siyo,” alihoji Osiah.