Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

TFF: Mapinduzi ya Simba ni batili

Muktasari:

 Mwenyekiti Kamati ya Katiba, Sheria na Hadhi za wachezaji, Alex Mgongolwa amepinga mapinduzi yaliyofanywa na wanachama wa Simba kwa madai ni batili na waliofanya hawakufuata katiba na kusisitiza kuwa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) halitambui kamati za muda za Simba zilizoundwa na waliofanya mapinduzi.

Wiki iliyopita baadhi ya wanachama wa Simba walifanya mkutano na kuupindua uongozi wa mwenyekiti Ismail Aden Rage aliyekuwa India kwa matibabu.

Kamati ya Mgongolwa ilikutana juzi kujadili suala hilo na kubaini kuwa kwa mujibu wa Ibara ya 22(2) ya Katiba ya Simba, Mkutano Mkuu wa Dharura unaitishwa na Kamati ya Utendaji baada ya wanachama wasiopungua 500 kuwasilisha ombi hilo kwa maandishi na kujiorodhesha kitu ambacho hakikufanyika.

Akizungumza jana Katibu Mkuu wa TFF, Angetile Osiah alisema Kamati hiyo ya Katiba, Sheria na Hadhi za wachezaji ilifikia uamuzi huo chini ya kifungu cha sheria ibara ya 22( 2) inayohusu mkutano mkuu wa dharura na kwa mujibu wa katiba rais wa klabu ndiye mwenye jukumu la kuitisha mkutano na siyo wanachama wake.

Osiah alisema kwa mujibu wa Katiba ya Simba wanachama hawaruhusiwi kuitisha mkutano na katika kikao hicho kamati imehoji ni kwa nini wamefanya hivyo na waliohudhuria mkutano huo hawakuhakikiwa kisheria.