Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

TFF, Yanga na Simba zaomboleza kifo cha shabiki

Dar es Salaam. Baada ya jana Wizara ya Afya kutoa taarifa ya kifo cha shabiki mmoja wa Yanga na wengine 29 kujeruhiwa, uongozi wa klabu ya Yanga, Simba na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kwa nyakati tofautI wametuma salamu za pole kwa familia ya shabiki huyo na majeruhi.

Taarifa ya kifo chake zilithibitishwa jana na Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu na baadae Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo alipoenda hospitali ya Temeke alitoa taarifa kuwa hadi sasa ni majeruhi 10 wanaendelea kupatiwa matibabu.

Rais TFF, Wallace Karia ni miongoni mwa viongozi waliotuma salamu hizo za pole kupitia ukurasa wa mitandao ya kijamii wa TFF.

"Rais Karia kwa niaba ya TFF ametoa pole kwa familia ya marehemu kwa msiba huo. Aidha ametoa pole kwa majeruhi wengine ambao wamelazwa hospitali ya Temeke na kuwatakia afya yao kutengamaa mapema ili warudi katika majukumu yao ya kila siku."

Uongozi wa Simba kupitia Idara ya Habari na Mawasiliano jana iliandika kwenye mtandao wa Instagram na kusikitishwa na taarifa za msiba wa shabiki huyo.

"Kwa masikitiko makubwa klabu ya Simba inatoa pole kwa familia ya shabiki aliyefariki uwanjani wakati akiwa katika jitihada za kushuhudia mechi ya fainali tunamuombea marehemu alazwe mahala pema peponi na majeruhi wapate ahueni haraka,"

Kwa upande wa Yanga kupitia chini ya Rais, Mhandisi Hersi Said wameandika hivi; "Uongozi wa Yanga umepokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya kufariki kwa shabiki mmoja wakati akiwa katika jitihada za kuingia ndani ya Uwanja uongozi unatoa pole kwa familia ya msiba na waliojeruhiwa mungu awaponye haraka,"

Yanga jana ilipoteza nyumbani Uwanja wa Mkapa kwa mabao 2-1 dhidi ya USM Alger kwenye mkondo wa kwanza wa fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Mchezo wa mkondo wa pili utachezwa nchini Algeria June 3 mwaka huu huku USM wakitanguliza mguu mmoja mbele wa kutwaa ubingwa huo.