Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

TFF yawapa angalizo wagombea Uchaguzi Mkuu

Muktasari:

  • Kamati ya Uchaguzi ya TFF, mwishoni mwa wiki iliyopita ilitangaza tarehe ya Uchaguzi Mkuu wa Shirikisho hilo kuwa ni Agosti 16, 2025.

Wakati zoezi la uchukuaji na urejeshaji fomu za kuwania nafasi tofauti za uongozi katika Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) likianza jana Jumatatu, Juni 16, 2025, Shirikisho hilo limewataka watia nia kuhakikisha wana kanuni za uchaguzi huo.

Uchaguzi huo utafanyika Agosti 16, mwaka huu na TFF imewapa angalizo watia nia ya kugombea kuzingatia kanuni.

“Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linawataka waombaji uongozi wote kuhakikisha wanakuwa na Kanuni za Uchaguzi. Hivyo wanapochukua fomu za kuwania uongozi katika uchaguzi huo utakaofanyika Agosti 16 mwaka huu kuhakikisha wanapata na kanuni za uchaguzi huo.

“Kwa wale ambao tayari wameshachukua fomu, wanatakiwa kuwasiliana na Sekretarieti ya TFF ili kupata Kanuni hizo.

“Nafasi zinazowaniwa katika uchaguzi huo utakaoendeshwa na Kamati ya Uchaguzi ya

TFF ni saba. Nafasi hizo ni Rais, na wajumbe sita wa Kamati ya Utendaji. Mwisho wa kuchukua na kurdisha fomu ni saa 10 kamili jioni Juni 20 mwaka huu. Fomu zinarudishwa katika ofisi za TFF,” imefafanua taarifa ya TFF.

Baada ya zoezi la kuchukua na kurudisha fomu kukamilika, Juni 21 hadi 23 mwaka huu ni muda wa kikao cha mchujo wa awali wa wagombea na kuandika barua za kuwajulisha wagombea juu ya mchujo wa awali.

Kuchapisha na kubandika kwenye mbao za matangazo orodha ya awali ya wagombea ni Juni 24 hadi 25, 2025.

Juni 26 hadi 28 mwaka huu ni kipindi cha kupokea na kuweka pingamizi kwa wagombea na kuanzia Juni 28 hadi 30 mwaka huu kutasikilizwa mapingamizi.

Usaili wa wagombea utafanyika Julai Mosi hadi 3, 2025 na Julai 4 hadi 5 ni muda wa kutangaza na kubandika kwenye mbao za matangazo matokeo ya awali ya usaili.

Sekretarieti itawakilisha masuala ya kimaadili kwenye kamati ya maadili, Julai 6 hadi 8 mwaka huu na siku nne zitakazofuata ni za kupokea, kusikiliza na kutolea uamuzi masuala ya kimaadili.

Baada ya hapo hatua mbalimbali zitaendelea kama zilivyoainishwa na Kamati ya Uchaguzi hadi siku ya zoezi lenyewe, Agosti 16.