Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Tunisia, Nigeria zaijazia mastaa Taifa Stars

Muktasari:

  • Taifa Stars katika fainali za AFCON 2025 itafungua dimba kwa kucheza na Nigeria, kisha itaikabili Uganda na itamaliza kwa kucheza na Tunisia.

Tunisia na Nigeria ambazo zimepangwa kundi moja na timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' katika Fainali za Mataifa ya Afrika (AFCON) 2025, zimeweka hadharani vikosi vyao vya mwisho kwa ajili ya mashindano hayo huku zikijaza nyota wanaocheza soka la kulipwa katika Ligi kubwa barani Ulaya.

Hannibal Mejbri anayechezea Burnley inayoshiriki Ligi Kuu England (EPL) ni mfano wa majina makubwa ambayo yamejumuishwa katika kikosi cha Tunisia chini ya Kocha Mkuu, Samy Trabelsi.

Trabelsi pia amewaita kundi nyota watatu wanaocheza katika Ligi Kuu Ujerumani 'Bundesliga' ambao ni Ismael Gharbi na Elias Saad wanaochezea Augsburg pia kuna Ellyes Skhiri wa Eintracht Frankfurt.

Kocha Trabelsi pia ametoa fursa kwa nyota wanaocheza soka ndani ya Afrika wakiongozwa na kipa mzoefu, Bechir Ben Saïd wa Esperance.

Kikosi cha Tunisia kwa AFCON 2025 kinaundwa na makipa, Aymen Dahmen (CS Sfaxien)

Bechir Ben Saïd (Espérance de Tunis), Sabri Ben Hassen (Étoile du Sahel) na Noureddine Farhati (Stade Tunisien).

Mabeki walioitwa ni Yan Valery (Sheffield Wednesday), Mohamed Ben Ali (Espérance de Tunis), Dylan Bronn (Servette FC), Montassar Talbi (FC Lorient), Yassine Meriah (Espérance de Tunis), Adem Arous (Kasimpasa), Nader Ghandri (Akhmat Grozny), Mortadha Ben Ouanes (Kasimpasa), Ali Abdi (OGC Nice) na Ali Maaloul (CS Sfaxien).

Viungo ni Ferjani Sassi (Al Gharafa), Ellyes Skhiri (Eintracht Frankfurt), Houssem Tka (Espérance de Tunis), Mohamed Hadj Mahmoud (FC Lugano), Ismael Gharbi (Augsburg), Hannibal Mejbri (Burnley FC), Naim Sliti (Al Shamal) na Mohamed Ali Ben Romdhane (Al Ahly).

Wahambuliaji walioitwa ni Elias Saad (Augsburg), Elias Achouri (FC Copenhagen), Hazem Mastouri (Dinamo Makhachkala), Sébastien Tounekti (Celtic), Firas Chaouat (Club Africain) na Seifeddine Jaziri (Zamalek).

Kwa upande mwingine, Nigeria nayo imeweka hadharani kikosi chake ambacho kina zaidi ya asilimia 90 ya wachezaji wanaocheza soka la kulipwa Ulaya.

Mastaa hao wa Nigeria, wataongozwa na nyota wa Galatasaray, Victor Osimhen lakini pia yumo staa wa Atalanta, Ademola Lookman.

Kipa wa Singida Black Stars, Amas Obasogie ni miongoni mwa wachezaji ambao Kocha Mkuu wa Nigeria, Eric Chelle amewajumuisha kikosini.

Wanaounda kikosi hicho ni makipa Stanley Nwabali, Amas Obasogie na Francis Uzoho huku mabeki wakiwa ni Calvin Bassey, Semi Ajayi, Bright Osayi-Samuel, Bruno Onyemaechi, Chidozie Awaziem, Zaidu Sanusi, Igoh Ogbu na Ryan Alebiosu.

Viungo ni Alex Iwobi, Frank Onyeka, Wilfred Ndidi, Raphael Onyedika, Tochukwu Nnadi, Fisayo Dele-Bashiru, Ebenezer Akinsanmiro na Usman Muhammed.

Kundi la washambuliaji lina Chidera Ejuke, Akor Adams, Ademola Lookman, Samuel Chukwueze, Victor Osimhen, Moses Simon, Paul Onuachu, Cyriel Dessers na Salim Fago Lawal