Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

UEFA ni usiku wa kisasi London

Muktasari:

  • Miji mbalimbali Ulaya itashuhudiwa vigogo wakitoana jasho na miongoni mwa mechi zinazosubiriwa kwa hamu ni zitakazopigwa katika majiji ya Madrid na London.

Madrid, Hispania. Baada ya wikiendi ya burudani ya soka kuacha vilio na furaha. Sasa ni zamu ya Ligi ya Mabingwa Ulaya jana zilipigwa mechi nane na matokeo ni kama mlivyosikia huku leo Jumatano kukiwa na vita kubwa ni nani atakaa kileleni na mechi tisa zitapigwa.

Miji mbalimbali Ulaya itashuhudiwa vigogo wakitoana jasho na miongoni mwa mechi zinazosubiriwa kwa hamu ni zitakazopigwa katika majiji ya Madrid na London.

Katika Jiji la London, kuna vita ya kisasi na Arsenal itaikaribisha Bayern Munich kuanzia saa 5:00 usiku katika dimba la Emirates.

Mechi hiyo itakuwa ya 14 kwa timu hizo kukutana Ligi ya Mabingwa Ulaya tangu mara ya kwanza mwaka 2000 na itakuwa pia  ni vita ya kuwania nani atakaa kileleni kwenye msimamo na zote zina nafasi ya kufanya hivyo zikiwa na pointi 12 sawa na Inter Milan, lakini zikipishana kwa tofauti ya mabao ya kufunga na kufungwa.

Mara ya mwisho timu hizi kukutana ni Aprili, 2024 na Arsenal ilitupwa nje ya michuano hiyo katika hatua ya robo fainali na kati ya mara zote 14 zilipokutana, Bayern imeshinda nane, sare tatu na washika mitutu hao wakishinda mara tatu.

Sare kwa timu hizo ni furaha kwa Inter na inaombea hilo litokee huku yenyewe ipate ushindi dhidi ya Atletico Madrid kwenye Uwanja wa Wanda Metropolitano kuanzia 5:00 usiku na kupanda kileleni ikifikisha pointi 15.

Atletico ambayo inashikilia nafasi ya 17 na pointi sita hii itakuwa ni mara yao ya tatu kukutana na Inter Milan katika historia ya Ligi ya Mabingwa na mara mbili walizokutana ilikuwa ni msimu wa 2023/24 katika raundi ua 16 bora na Inter ilisonga mbele kwa changamoto ya mikwaju ya penalti baada ya mechi sare katika matokeo ya jumla.

Mbali ya mechi hizi, mabingwa wa kihistoria wa taji hili, Real Madrid itavaana na Olympiacos ya Ugiriki ugenini, huku bingwa mtetezi PSG ikiikaribisha Tottenham jijini Paris.

Liverpool itakuwa Anfield kuumana na PSV, Sporting Lisbon itakipiga dhidi ya Club Brugge ya Ubelgiji na Frankfurt itaialika Atalanta kutoka Italia na mechi hizi zitaanza saa 5:00 usiku.

Mechi ya mapema leo ni Copenhagen dhidi ya Kairat itayoanza saa 2:45 usiku.