Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Estevao ang'ara Chelsea ikiichapa Barcelona, Man City hoi nyumbani

CHELSEA Pict

Muktasari:

  • Estevao mwenye umri wa miaka 18, alifunga bao la pili la kuvutia, akimtoka beki Pau Cubarsi, kisha kumzidi nguvu Alejandro Balde na kumfunga kipa Joan Garcia kwa shuti la nguvu.

London, England. Winga wa Chelsea, Estevao Willian, ameng'ara usiku wa Novemba 25, 2025 wakati timu hiyo ikipata ushindi wa 3-0 dhidi ya Barcelona iliyokuwa na wachezaji 10 katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya iliyochezwa Stamford Bridge.

Estevao mwenye umri wa miaka 18, alifunga bao la pili la kuvutia, akimtoka beki Pau Cubarsi, kisha kumzidi nguvu Alejandro Balde na kumfunga kipa Joan Garcia kwa shuti la nguvu. Bao hilo lilikuja muda mfupi baada ya nahodha wa Barcelona, Ronald Araujo, kutolewa kwa kadi nyekundu baada ya kuonyeshwa kadi ya pili ya njano kabla ya kipindi cha kwanza kumalizika.

Chelsea ilikuwa tayari ipo mbele kwa bao moja baada ya kujifunga kwa beki wa Barcelona, Jules Kounde kufuatia kona fupi iliyoandaliwa na Estevao, Alejandro Garnacho na Marc Cucurella.

Liam Delap aliyeingia akitokea benchi alikamilisha ushindi huo kwa kufunga bao la tatu, likiwa ni bao lake la kwanza msimu huu na kuvunja ukame wa mechi 11 bila kufunga.

Katika mechi hiyo, Estevao aliwazidi maarifa nyota mwenzake wa Barcelona, Lamine Yamal, pia mwenye miaka 18, ambaye alicheza bila makali na baadaye kubadilishwa dakika ya 80 huku mashabiki wa Chelsea wakimzomea. Dakika mbili baadaye, kocha wa Chelsea, Enzo Maresca alimtoa Estevao na kumpa heshima ya kusindikizwa kwa shangwe kutoka kwa mashabiki.

Chelsea ilimkosa nyota wake tegemeo, Cole Palmer kutokana na jeraha la kidole, lakini kikosi hicho kiliendelea kuonyesha ubora. 

CHEL 01

Enzo Fernandez angeweza kufunga mabao mawili ya mpira wa adhabu lakini yalikataliwa kwa kuotea, huku Reece James akilazimisha kipa kufanya kazi mara mbili kutokana na mashuti ya mbali.

Barcelona ilikosa nafasi yao bora kipindi cha kwanza baada ya mshambuliaji wa zamani wa Manchester City, Ferran Torres, kukosa kwa karibu, kabla ya kubadilishwa kipindi cha pili na kuingia Marcus Rashford aliyeko kwa mkopo kutoka Manchester United. Hata hivyo, Rashford hakuweza kuisaidia Barcelona kubadilisha matokeo.

Estevao alifunga bao la pili kwa juhudi binafsi kabla ya Delap kufunga la tatu akimalizia pasi ya Fernandez aliyewazidi ujanja walinzi wa Barcelona. 

Ushindi huo umeipandisha Chelsea hadi nafasi ya nane kwenye ligi ya timu 36, jambo linalomaanisha kuwa inaweza kuepuka mechi za mtoano za mwezi Februari 2026 endapo itaendelea kusalia nafasi nane za juu, huku ikibaki na mechi tatu za kucheza.


CHEL 02

MAN CITY HOI
Mechi ya 100 ya Pep Guardiola kama kocha wa Manchester City katika Ligi ya Mabingwa Ulaya haikuenda kama ilivyotarajiwa, baada ya kikosi hicho kilichofanyiwa mabadiliko makubwa kupigwa 2-0 na Bayer Leverkusen nyumbani kwenye Dimba la Etihad.

Guardiola alifanya mabadiliko 10 kwenye kikosi kilichoanza, kufuatia kipigo cha Ligi Kuu dhidi ya Newcastle, lakini hatua hiyo ilimgeukia na kuzaa maafa, huku City ikikumbana na kipigo cha pili mfululizo.

City ilianza kwa kasi na ilikaribia kufunga mapema kupitia shuti la Nathan Ake lakini kipa Mark Flekken aliokoa kwa ustadi. Hata hivyo, baadaye City ilionekana kucheza kwa mwendo wa taratibu na bila ubunifu mkubwa.

Leverkusen ilionyesha kasi katika mashambulizi ya kushtukiza na ilipata bao la kuongoza kupitia nahodha Alejandro Grimaldo aliyemalizia kwa ustadi pasi ya Christian Kofane.

Wachezaji wa akiba wa City walionekana kukosa maelewano na walishindwa kuunganisha mashambulizi ya maana. Tijjani Reijnders alipenya vizuri lakini shuti lake lilidakwa na Flekken.

CHEL 03

Ndoto ya Leverkusen iliendelea dakika ya 54 wakati mshambuliaji wa Czech, Patrik Schick, alipofunga kwa kichwa baada ya kupokea krosi safi kutoka kwa Ibrahim Maza.

Nyota wa City, Erling Haaland, aliingia dakika ya 60 na karibu afanye maajabu dakika 10 baadaye alipounganishwa na Phil Foden, lakini Flekken tena alizuia kwa kuondoa mpira miguuni mwake.

Haaland alikosa tena nafasi nzuri aliposhindwa kulenga lango, huku mashabiki wa Leverkusen wakishangilia kwa nguvu wakishuhudia ushindi muhimu ugenini.

MATOKEO MECHI ZA JANA
Ajax 0-2 Benfica
Galatasaray 0-1 Union Saint-Gilloise
Marseille 2-1 Newcastle
Bodø/Glimt 2-3 Juventus
Napoli 2-0 Qarabag FK
Dortmund 4-0 Villarreal
Chelsea 3-0 Barcelona
Man City 0-2 Leverkusen
Slavia Praha 0-0 Athletic Club