VIDEO-Mkurugenzi wa MCL, Naibu Spika wang’ara Mbeya Tulia Marathon

Muktasari:
- Naibu Spika Dk, Tulia ameipongeza MCL kujitosa kudhamini mbio za Mbeya Tulia Marathoni. Mbali na kudhamini wafanyakazi wa MCL wakiongozwa na Mkurugenzi wao, walimaliza mbio za km 5.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Mwananchi Communications Limited (MCL), Francis Nanai na Naibu Spika Ackson Tulia wamemaliza mbio za Mbeya Tulia Marathoni katika kundi la kwanza kwenye mbio za kilomita 5.
Naibu Spika Dk, Tulia ameipongeza MCL kujitosa kudhamini mbio za Mbeya Tulia Marathoni. Mbali na kudhamini wafanyakazi wa MCL wakiongozwa na Mkurugenzi wao, walimaliza mbio za km 5.
Wanariadha wengine wa MCL waliomaliza mbio hizo ni Audax Kamala, Philipo Ringo, Hosea Kimani na Deus Turyamuseeba (km 21) na Jackson Ngasa aliyemaliza km 5.
Pia Mkuu wa Kitengo cha Michezo MCL, Ndaya Kasongo na Meneja Masoko, Sarah Munema pia walimaliza km 5, huku Angetile Osiah akikimbia kilometa 2.