Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Video: Mpole aikataa Simba, anukia kusaini nje

Muktasari:

  • KINARA wa upachikaji wa mabao msimu uliopita kwenye Ligi Kuu Bara, Mshambuliaji wa Geita Gold George Mpole amefunguka sababu za kushindwa kusaini Simba ni suala la maslahi tu.

KINARA wa upachikaji wa mabao msimu uliopita kwenye Ligi Kuu Bara, Mshambuliaji wa Geita Gold George Mpole amefunguka sababu za kushindwa kusaini Simba ni suala la maslahi tu.

Mpole ambaye tayari ameongeza mkataba wa mwaka mmoja kuendelea kuitumikia Geita Gold amesema ni kweli alipokea ofa kutoka Simba lakini walikidhi maslahi yake ndio maana hakuona umuhimu wa kuondoka klabuni hapo.

#EXCLUSIVE: MPOLE afunguka kuikimbia SIMBA | Geita wampa anachotaka

“Nilikuwa na ofa nyingi kutoka timu za ndani na nje ya Tanzania ila nimeamua kubaki kwa sababu wameweza kunitimizia mahitaji yangu.” amesema Mpole na kuongeza;

“Kuhusu kuzungumzwa kwamba nimechelewa kusaini mkataba na Geita Gold sio kweli, ni timu ambayo nashirikiana nayo kwenye kila kitu na suala la ofa zangu za nje taarifa hizo wanazo,” amesema.

Nyota huyo alikuwa sehemu ya kikosi cha Geita katika mchezo wa kwanza wa ufunguzi Ligi Kuu Bara wakati timu yake ilipofungwa mabao 3-0 dhidi ya Simba jana kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa.