Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Waarabu kumng’oa Alexander Isak Newcastle United

Muktasari:

  • Mkataba wa Alexander Isak na Newcastle United utafikia tamati Juni 30, 2028.

Al Hilal ya Saudi Arabia imeamua kujitosa katika vita ya kumuwania Alexander Isak ambaye inaripotiwa ameiambia Newcastle United kuwa anataka kutafuta changamoto mpya kwingine.

Miamba hiyo ya Saudi Arabia imepanga kumlipa Alexander Isak mshahara wa Pauni 600,000 (Sh2.1 bilioni) kwa wiki ikiwa nyota huyo wa Newcastle United atakubali kujiunga nayo katika dirisha linaloendelea la usajili la majira ya kiangazi.

Kiwango hicho cha mshahara ambacho Isak atapokea ni baada ya makato ya kodi ambapo kitakuwa ni mara tano ya kile anachopokea hivi sasa ndani ya Newcastle United ambapo kwa wiki analipwa Pauni 120,000 (Sh412 bilioni).

Kwa sasa Isak hayupo katika kikosi cha Newcastle United ambacho kimeweka kambi ya maandalizi ya msimu mpya huko Asia na hivi karibuni aliripotiwa kuuambia uongozi wa timu yake kuwa anataka kuondoka klabuni hapo.

Ni Liverpool tu kwa timu za England ambayo inaonekana kutamani huduma ya mchezaji huyo kutokana na kiasi kikubwa cha fedha ambacho Newcastle United inakihitaji ili imruhusu mshambuliaji huyo kupata changamoto mpya kwingine.

Inaripotiwa kwamba Newcastle United ipo tayari kukaa mezani na timu nyingine kujadili uhamisho wa Isak ikiwa ofa itakayoletwa itaendana na matakwa yao kwa maana ya kiasi cha Pauni 150 milioni (Sh515 bilioni) ili kumuachia mchezaji huyo.

Na Al Hilal ndio inawezekana ikawa katika nafasi kubwa ya kumnyakua nyota huyo mwenye umri wa miaka 25 kwa vile ipo tayari kulipa kiasi cha fedha kinachohitajika

Kiwango cha mshahara ambacho Isak atalipwa kwa wiki ndani ya Al Hilal kitamfanya aingie katika orodha ya nyota wa soka 10 wanaolipwa kiasi kikubwa cha fedha duniani.

Isak amekuwa ni miongoni mwa nyota tishio wa kufumania nyavu katika miaka ya hivyo karibuni tangu alipojiunga na Newcastle United mwaka 2022 akitokea Real Sociedad ya Hispania.

Katika miaka minne aliyoitumikia Newcastle United, Isak amefumania nyavu mara 62 kwa mechi 109 huku akipiga pasi za mwisho 11.