Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Waarabu wanavyoitibulia Simba CAF 

Muktasari:

  • Kwenye Mashindano ya Kombe la Shirikisho Afrika, Simba imecheza michezo saba ikiwa ugenini dhidi ya timu za Waarabu ambapo imepata sare michezo miwili huku ikipoteza michezo mitano.

Dar es Salaam. Simba imeendelea kukumbana na changamoto kubwa inapokutana na timu za Kiarabu kwenye mashindano ya kimataifa, timu hizo zinazotoka ukanda wa Kaskazini mwa Afrika zimekuwa mwiba mchungu kwa Wekundu wa Msimbazi zikiwanyima nafasi ya kufika mbali katika mashindano hayo.

Kwenye Mashindano ya Kombe la Shirikisho Afrika, Simba imecheza michezo saba ikiwa ugenini dhidi ya timu za Waarabu ambapo imepata sare michezo miwili huku ikipoteza michezo mitano.

Kwenye michezo minne ambayo Simba ilipoteza ugenini miwili ilicheza Algeria ikipoteza kwa mabao 3-1 dhidi ya ES Sétif, Aprili 6, 2012 huku mwingine ikipoteza Desemba 8, 2024 ilipofungwa mabao 2-1 dhidi ya CS Constantine.

Michezo mingine ambayo Simba ilipoteza ugenini ilikuwa Mei 8, 2010 ilipofungwa mabao 5-1 dhidi ya Haras El-Hadood ya Misri, Mei 13, 2012 ilipoteza ugenini mabao 3-0 dhidi ya Al-Ahly Shendi ya Sudan, huku mara ya mwisho kwenye Kombe la Shirikisho Simba ilipoteza Uarabuni Februari 27, 2022 ilipofungwa mabao 2-0 dhidi ya RS Berkane ya Morocco.

Katika michezo minne ambayo Simba ilipoteza ugenini vilevile ilifanikiwa kupata ushindi ilipokuwa nyumbani ambapo mara ya mwisho ilicheza na Al Ahli Tripoli ya Libya ikiifunga mabao 3-1, Septemba 22, 2024 huku mechi ya mwisho kwenye makundi ilicheza dhidi ya RS Berkane ikishinda bao 1-0, Machi 13, 2022.

Simba ilipata sare dhidi ya Al-Masry kwenye michezo yote miwili iliocheza nyumbani na ugenini ambapo Machi 7, 2018 ilipata sare ya mabao 2-2 kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam kabla ya kwenda Misri Machi 17, 2018 ilipolazimishwa sare ya 0-0 kama ilivyofanya dhidi ya Al Ahli Tripoli Septemba 15, 2024.


Kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika

1994 Simba ilitolewa kwenye hatua ya nusu fainali na Klabu ya El-Mahalla kutoka Misri kwa mikwaju ya penalti baada ya timu zote mbili kupata ushindi wa bao 1-0 zikiwa nyumbani.

2003, Simba ilitolewa kwenye hatua ya makundi huku ikipoteza mechi dhidi ya Ismaily ya Misri ambapo ilifungwa mabao 2-1 ugenini wakati nyumbani ilitoa sare ya 0-0, ikimaliza nafasi ya tatu kwenye kundi A ambapo nafasi ya kwanza ilishikwa na Enyimba iliyokuwa na pointi 12, nafasi ya pili ilishikwa na Ismaily iliokuwa na pointi 11, nafasi ya tatu ilishika Simba ikiwa na pointi saba huku nafasi ya nne ilishikwa na ASEC Mimosas iliokuwa na pointi nne.

2011, Simba iliondolewa na Wydad Casablanca katika hatua za mtoano ilipokubali kipigo cha mabao 3-0 huku mwaka 2018, ikifungwa na Al Ahly ya Misri mabao 5-0 ugenini kwenye hatua ya makundi ambapo ilishinda bao 1-0 ikiwa nyumbani.

Msimu wa 2020-2021 Simba ilifungwa bao1-0 ugenini na Al Ahly kwenye hatua ya makundi huku yenyewe ikishinda bao 1-0 kwenye uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam ambapo iliongoza kundi baada ya kukusanya pointi 13.

Msimu wa 2022-2023, Simba ilikutana na Raja Casablanca kwenye hatua ya makundi ambapo ilifungwa katika mechi zote mbili walizokutana ambapo mechi ya kwanza Simba ilifungwa mabao 3-0 ikiwa nyumbani wakati mechi ya pili ilikubali kipigo cha mabao 3-1 ugenini.

Simba ilifanikiwa kwenda hatua ya robo fainali baada ya kukusanya pointi tisa ambako napo ilikutana na Whydad Casablanca ambayo iliwatoa kwa changamoto za mikwaju ya penalti baada ya timu zote mbili kushinda bao 1-0 zilipokuwa nyumbani.

Msimu wa 2023-2024, ilikutana na Whydad Casablanca kwenye makundi ambapo Simba ilipoteza bao 1-0 ikifungwa dakika za mwisho ikiwa ugenini. Simba ilifanikiwa kwenda hatua ya robo fainali ambapo ilikutana na Al Ahly ya Misri ambayo iliifunga Simba nyumbani na ugenini ikifungwa nyumbani 1-0 na ugenini ilifungwa 2-0.

Msimu huu kwenye Kombe la Shirikisho Afrika Simba imepangwa kundi A ikiwa na pointi tatu katika nafasi ya pili, CS Constantine inaongoza kundi ikiwa na pointi sita wakati Bravos inashika nafasi ya tatu ikiwa na pointi tatu huku CS Sfaxien ikibuluza mkia ikiwa haina pointi.