Wachezaji nyota waliosajiliwa, kuachwa msimu huu Ligi Kuu

Hamis Kiiza wa Simba SC
Muktasari:
- Usajili unafungwa leo saa 6 usiku
- Kwa mujibu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), endapo kuna klabu itachelewesha kuleta usajili wake kuanzia siku dirisha lilipofungwa hadi Agosti 30, itatozwa kiasi cha Sh500,000 kwa kila mchezaji itakayemsajili.
Dar es Salaam. Wakati dirisha la usajili likifungwa leo saa 6 usiku klabu mbalimbali zikiwa zimekamilisha harakati zao za usajili tayari kwa kuanza msimu mpya wa ligi hiyo.
Kwa mujibu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), endapo kuna klabu itachelewesha kuleta usajili wake kuanzia siku dirisha lilipofungwa hadi Agosti 30, itatozwa kiasi cha Sh500,000 kwa kila mchezaji itakayemsajili.
Mwisho wa kufanya uhamisho wa kimataifa wa wachezaji kwa njia ya mtandao TMS ni Septemba 6.
Hata hivyo Mwananchi imeangalia baadhi ya wachezaji waliosajili hadi jana jioni.
Yanga
Waliosajiliwa: Benedictor Tinocco (Kagera Sugar), Mwinyi Haji (KMKM), Vincent Bossou (Togo), Thabani Kamusoko, Donald Ngoma (wote Platnum, Zimbabwe), Geofrey Mwashiuya (Kimondo), Deus Kaseke (Mbeya City), Antony Mateo Saimon, Mudathir Khamis (wote KMKM) na Malimi Busungu (Mgambo JKT).
Walioachwa: Nizar Khalfan, Jerry Tegete, Hassan Dilunga, Said Bahanuzi, Danny Mrwanda, Omega Seme na Hamis Thabit, Mrisho Ngassa (Huru kwenda Free State, Afrika Kusini).
Mkopo: Edward Charles (JKT Ruvu), Rajab Zahir (anatarajiwa kutolewa mkopo Stand United) na Hussein Javu (anatarajiwa kutolewa kwa mkopo Mtibwa Sugar).
Simba
Waliosajiliwa: Emiry Nibomana (Burundi), Samir Haji Nuhu (Huru), Mohammed Faki (JKT Ruvu), Justice Majabvi (Zimbabwe), Mwinyi Kazimoto( Al Markhiya Qatar), Peter Mwalyanzi (Mbeya City),Hamis Kiiza (Uganda), Mussa Mgosi (Mtibwa Sugar), Vincent Angban (Ivory Coast) na Kevin Ndayisenga (Burundi).
Waliochwa: Ibrahim Twaha, Willium Lucian’Gallas’, Amri Kiemba, Nassor Masoud ‘Chollo’, Abdallah Seseme, Ivo Mapunda, Ramadhani Singano ‘Messi, Hussen Sharrif ‘Casilas’ na Elius Maguri.
Azam
Waliosajiliwa: Ramadhani Singano (Simba), Ame Ali (Mtibwa), Allan Wanga (El Merreikh, Sudan), na Jean Mugiraneza ‘Migi’ (APR Rwanda).
Waliowaacha: Gaudence Mwaikimba, Samir Haji Nuhu, Brian Majwega na David Mwantika.
Mbeya City
Waliosajiliwa: Joseph Mahundi (Coastal Union), Gideon Benson(Ndanda), James Ambrose (Polisi Morogoro) na Haruna Shamte (JKT Ruvu).
Walioachwa: Peter Mwalyanzi, Deus Kaseke, Antony Matogolo, Peter Mapunda, David Burhan, Saad Kipanga, Paul Nonga na Deo Lucas.
Coastal Union
Waliowasajili: Abasalim Chidebele (Stand United), Adeyum Salehe (JKU) Nasoro Kapama(Ndanda), Ernest Mwalupani (Ndanda), Yassin Mustapa Salim (Stand United), Sultan Juma (African Sports), Ahmed Shiboli (African Sports), Mohamed Hamis Mititi (Huru), Benedict Haule (Huru), Ismail Mohamed Suma (Stand United), Patrick Protas Kamuhagile (Huru), Jackson Sabweto (SC Villa, Uganda), Yossouph Sabo (Younde FC, Cameroon).
Waliowaacha: Shabani Kado, Keneth Masumbuko, Yayo Kato Lutimba, Seleimani Kibuta, Razack Khalfani, Itubu Imbem, Othumani Tamimu, Hussein Sued, Mansour Alawi, Amani Juma, Mohamedi Mtindi na Mohamed Hassani, Rama Salim, na Joseph Mahundi.
Prisons
Waliowasajili: Juma Seif Kijiko (Ruvu Shooting), Cosmas Lewis (Prisons).
Waliowaacha: Jimmy Shoji, Ibrahim Mamba
Mtibwa Sugar
Waliowasajili: Hussein Sharrif (Simba), Idrisa Rashid (Simba), Said Bahanuzi (Yanga) na iko mbioni kumchukua Hussin Javu kwa mkopo kutoka Yanga.
Waliowaacha: Ame Ali, Mussa Hassan Mgosi, David Luhende.
JKT Ruvu
Waliowasajili: Saady Kipanga (Mbeya City), Gaudence Mwaikimba(Azam), Mateo Daniel (Kimondo), Tony Kavishe (Polisi Moro), Amour Janja (JKU), Michael Aidan (Ruvu Shooting).
Waliowaacha: Damas Makwaya, Haruna Shamte, Jabir Aziz na Juma Nade.
Stand United
Waliowasajili: Said Nassoro ‘Cholo (Simba), Haruna Chanongo (Huru), Hamad Ndikumana (Rwanda), Amri Kiemba (Simba), Hassan Dilunga (Yanga), Seleman Kassim ‘Selembe’ (Polisi Moro) na Jacob Massawe (Ndanda).
Waliowaacha: Abasalim Chidebele, Salehe Mohamed, Yassin Mustapa Salim na Mohamed Suma.
Ndanda
Waliowasajili: Atupele Green (Kagera Sugar), Juma Nade (JKT Ruvu), Willium Lucian ‘Gallas’ (Simba), Ibrahim Mamba (Prisons), Salvatory Ntebe (Ruvu Shooting), Mustapha Mbarouk, Meshack Fredrick.
Waliowaacha; Stahamil Mbonde, Jacob Massawe, Ernest Mwalupani, Nassor Kapama, Wilibert Mweta na Gideon Benson.
Kagera Sugar
Waliowasajili: Abou Hasheem (African Lyon), Lambere Jerome (Ruvu Shooting), Saleh Mohamed (Stand United), Deo Lucas (Mbeya City) na Jimmy Shijo (Prisons).
Waliowaacha: Rashid Mandawa, Maregesi Mwanga, Atupele Green, Benedictor Tinocco.
Mwadui:
Waliowasajili: Shaban Kado (Coastal Union), Anthon Matogolo (Mbeya City),Jabir Aziz(JKT Ruvu), David Luhende (Mtibwa Sugar), Razack Khalfan(Coastl Union). Nizar Khalfan(Yanga), Paul Nonga (Mbeya City), Rashid Mandawa (Kagera Sugar), Malegesi Mwangwa (Kagera Sugar), Jamal Mnyate na Malika Ndeule.
African Sports
Waliowasajili: Ali Shiboli (African Sports), Nsa Job (Huru), Zahoro Pazi(Huru) na Bakari Masoud (Huru)Toto African.
Waliowasajili: Abdallah Seseme (Simba), Edward Christopher (Polisi Morogoro), Hassan Khatibu (Friends Rangers), Japhet Nzegati, Miraji Athuman, Bakili Junior, Waziri Hamad na Hussein Chuko.
Majimaji
Waliowasajili: David Burhan (Mbeya City), Peter Mapunda (Mbeya City), Godfrey Taita (Villa Squad), Kelvin Friday (Azam).
Mgambo Shooting
Klabu hii ya jeshi msimu huu usajili wake umekuwa siri kubwa.