Wachezaji Simba wapita wote vipimo vya covid 19

Friday March 05 2021
corona pic
By Thobias Sebastian

KHARTOUM, SUDAN. KWA nyakati tofauti katika mashindano ya Kimataifa kama Ligi ya mabingwa Afrika na mengineyo kunakuwa na madai ya figisu inapofika kwenye vipimo vya covid 19.

Kikosi cha Simba kilifanya vipimo hivyo jana Februari 4 asubuhi katika kambi yao hapa katika hoteli ya nyota tano ya Al Salam.

Majibu ya vipimo hayo yametoka na wachezaji, benchi la ufundi, viongozi na wote waliokuwa katika msafara majibu yao yametoka safi na hakuna mwenye maambukizi.

Kuwa safi kwa majibu hayo kazi inabaki kwa kocha wa Simba, Didier Gomes kuchagua wachezaji ambao anawataka kuwatumia katika mechi hiyo.

Ikumbukwe Simba walivyoenda kucheza ugenini dhidi ya AS Vita kukutwa na maambukizi ya virusi vya corona.

Advertisement