Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wachezaji wa kuchungwa Yanga vs AS FAR

Muktasari:

  • Huu utakuwa ni mwanzo wa Yanga kuitafuta hatua ya mtoano ambayo ilishindwa kufika msimu uliopita baada ya kulazimishwa suluhu kwenye Uwanja wa nyumbani na MC Alger ya Algeria.

Kesho Jumamosi Novemba 22, 2025 Yanga itashuka kwenye Uwanja wa New Amaan Complex, Visiwani Zanzibar kutupa karata yake ya kwanza katika hatua ya makundi ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu wa 2025/2026.

Katika mechi ya kesho Yanga itavaana na AS FAR ya Morocco katika kundi B ambalo linatimu nyingine za Al Ahly ya Misri na JS Kabylie ya Algeria.

Katika mchezo huo wa kusaka alama tatu muhimu utakaochezwa saa 10:00 jioni, Yanga inatakiwa kuhakikisha haiwapi nafasi ya kumiliki sana mpira wachezaji wa AS FAR kutokana na hatari kubwa waliyonayo hasa wakiwa karibu na lango.

Miongoni mwa wachezaji hatari ambao Yanga inapaswa kuwachunga katika mechi ya kesho ni naodha wa timu hiyo Mohamed Hrimat ambaye ni kiungo anayekaba pamoja na kushambulia.

Kiungo huyo hatari hadi sasa amehusika katika mabao sita kwenye Ligi Kuu ya Morocco maarufu kama Botola Pro ambapo amefunga matano na kutoa pasi moja ya bao.

Ikumbukwe Hrimat ndiyo yule kiungo ambaye alionyesha kiwango bora alipokuwa na timu ya Taifa ya Morocco katika mashindano ya Mataifa Afrika kwa wachezaji wa ndani CHAN 2024 yaliyofanyika Kenya, Uganda na Tanzania na yeye akaibuka kama mchezaji bora wa mashindano baada ya kuisaidia timu yake kubeba Ubingwa.

Ukiachana na huyo, yupo mwingine Youssef El Fahli ambaye aliibuka Mchezaji Bora wa Ligi Kuu ya Morocco mwezi uliopita.

El Fahli ni mshambuliaji hatari ambaye hadi sasa amethibitisha hilo kwa kupachika mabao manne na kutoa pasi moja ya bao kwenye Ligi Kuu. Mshambuliaji huyo na kiungo Hrimat ambaye ni naodha, wote wawili wameonekana kuwa moyo wa timu hiyo kutokana na mchango waliyoonyesha hadi sasa.

Nyota hao kwa ujumla wamechangia jumla ya mabao 11 kati ya 14 yaliyofungwa, wakifunga mabao tisa na kutoa pasi mbili za mabao katika mechi nane ambazo AS FAR imecheza kwenye ligi ya Morocco ikiwa inashika nafasi ya pili kwa pointi 18 nyuma ya vinara Wydad Casablanca wenye pointi 20.

Ukiachana na safu yao ya kiungo na ushambuliaji ambayo inaonekana kuimarika, vile vile kwenye upande wa kuzuia wapo vizuri kwani katika michezo minane iliyocheza, AS FAR imeruhusu bao moja pekee sawa na Raja Casablanca anayofundishwa na Fadlu Davids.

Hata hivyo, Yanga inaweza kukabiliana na changamoto ya wachezaji hao iwapo itahakikisha inaingia uwanjani kwa nidhamu ya kuwaheshimu wapinzania hao.

Uwepo wa Ibrahim Baka na Dickson Job kwenye eneo la ulinzi wa kati, unaipa faida timu hiyo kwani walinzi hao wawili si mara ya kwanza kuwakabili washambuliaji hatari.

Serhou Guirassy, mshambuliaji wa Borussia Dortmund ya Ujerumani aliweza kudhibitiwa na walinzi hao wa Yanga katika mechi ya makundi ya kuwania kufuzu michuano ya Mataifa Afrika (AFCON) mechi ambayo Taifa Stars ilishinda bao 1-0 na kufanikiwa kutinga kwenye mashindano hayo kwa mara ya pili mfululizo.

Mbali na walinzi hao, wapo wachezaji wengine hatari kama Pacome Zouzoua ambaye anauwezo wa kumiliki mpira na kuwasumbua walinzi wa timu pinzani, jambo linaloipa pia faida Yanga katika mchezo huo.

Huu utakuwa ni mwanzo wa Yanga kuitafuta hatua ya mtoano ambayo ilishindwa kufika msimu uliopita baada ya kulazimishwa suluhu kwenye Uwanja wa nyumbani na MC Alger ya Algeria.