Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wakimbiaji 300 washiriki mbio za Tazara,

Dar es Salaam. Zaidi ya wakimbiaji 300 kutoka klabu zaidi ya 20 za wakimbiaji jijini Dar es Salaam wameshiriki mbio maalum za barabarani zilizoandaliwa kwa ajili ya kuadhimisha miaka 50 ya Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA).

Mbio hizo zilizopewa jina la ‘Tazara @50 Fun Ran’ zilianzia na kumalizikia katika ukumbi wa Police Officers Messi, Oysterbay ambapo kulikuwa na mbio za kilometa tano, kumi na 15. 

Katibu wa Klabu ya The Runners Tanzania na mratibu wa tukio hilo, Godfrey Mwanakulia, amesema mbio hizo ziliandaliwa si kwa ajili ya kuadhimisha miaka 50 ya TAZARA pekee, bali pia kuhamasisha watanzania kuzingatia mazoezi kwa ajili ya afya bora.

"Lengo letu ni kuwahamasisha Watanzania kufanya mazoezi mara kwa mara. Kukimbia huimarisha afya ya mwili na akili, huongeza uwezo wa mapafu, hupunguza msongo wa mawazo na kuboresha utendaji wa ubongo," amesema Mwanakulia.

Mmoja wa washiriki wa mbio hizo, Hadija Kambenga, amepongeza mpango huo akisema michezo huchangia kujenga jamii yenye mshikamano huku ikiimarisha afya na ustawi wa wafanyakazi.

"Mazoezi huondoa msongo wa mawazo, huleta furaha na hata kuongeza ufanisi kazini. Tunawahimiza watu wote kushiriki shughuli za michezo kwa manufaa ya afya zao," amesema Hadija.

 Awali akizungumza katika mbio hizo, Mkurugenzi Mtendaji wa Tazara, Bruno Chinga'andu, amesema maadhimisho hayo ya jubilee ya dhahabu si tu ni ya kusherehekea mafanikio ya reli hiyo katika kipindi cha miaka 50 iliyopita, bali pia ni fursa ya kutazama malengo na dira ya baadaye.

"Tunasherehekea hatua tulizopiga kwa miaka 50 iliyopita huku tukitazama mustakabali wa Tazara.

“Tunaendelea kubadilika na kuwa njia ya kisasa ya reli itakayochochea biashara na ustawi wa uchumi wa kikanda," amesema Chinga'andu.

Aidha amesema mbio hizo zilikuwa sehemu ya mfululizo wa shughuli za kuelekea maadhimisho ya miaka 50 ya Tazara, zikilenga kuunganisha ari ya michezo, kuhamasisha afya bora kwa wafanyakazi na jamii kwa ujumla.

Pia ni pamoja na kuonyesha dhamira ya kuijenga Tazara ya kisasa itakayochochea maendeleo ya uchumi na ushirikiano wa kikanda.