Wananchi mdogo mdogo kwa Mkapa

Saturday August 06 2022
mdogo pic
By Thomas Ng'itu

MASHABIKI wa klabu ya Yanga wameanza kuingia mdogo mdogo katika uwanja wa Benjamin Mkapa kwa ajili ya kushuhudia mastaa wao wapya leo.

Yanga leo watakuwa na kilele cha Wiki ya Mwaananchi ambayo inatumika kwa ajili ya kuwatambulisha wachezaji wao wa msimu ujao huku wakicheza mchezo wa kirafiki na Vipers kutoka Uganda.

Mwanaspoti ambalo lipo katika Uwanja wa Mkapa limeshuhudia mashabiki wa Yanga wakiingia polepole uwanjani.

Mashabiki hao walikuwa wachache saa 5 asubuhi tofauti na siku zingine za nyuma. katika Tamasha la siku ya Mwananchi.

Hili ni tamasha la nne kwa Wananchi tangu waanze kufanya ikiwa ni sehemu ya kuwatambulisha mastaa watakaoitumikia timu yao katika msimu unaofuata.

Advertisement