Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wapongeza uhuru wa kamati Fifa

Sepp Blatter (kushoto) akiwa na Michel Platini.

Muktasari:

Blatter na Platini walifungiwa juzi kutojihusisha na masuala ya soka kwa miaka minane kutokana na uchunguzi uliofanywa na kamati ya maadili ya Fifa iliyobaini Fifa ilitoa rushwa ya Pauni 1.3 milioni kwenda kwa Platini na kuidhinishwa na Blatter.

Dar es Salaam. Uamuzi wa kufungiwa miaka minane kwa rais wa Shirikisho la Soka Kimataifa (Fifa), Sepp Blatter na mwenzake wa Shirikisho la Soka Ulaya (Uefa), Michel Platini umetafsiriwa kwa mitazamo tofauti na wadau wa soka nchini. Baadhi wametaka uhuru wa kamati za Fifa uwapo pia kwenye Shirikisho la Tanzania (TFF).

Blatter na Platini walifungiwa juzi kutojihusisha na masuala ya soka kwa miaka minane kutokana na uchunguzi uliofanywa na kamati ya maadili ya Fifa iliyobaini Fifa ilitoa rushwa ya Pauni 1.3 milioni kwenda kwa Platini na kuidhinishwa na Blatter.

Blatter na Platini walitiwa hatiani na kamati hiyo iliyokuwa chini ya Jaji Hans-Joachim Eckert baada ya kubainika walikiuka kanuni za kimaadili kwa kufanya malipo yenye mtazamo wa rushwa aliyolipwa Platini mwaka 2011. Blatter na Platini wamesema malipo hayo yalikuwa ni heshima kwa kazi nzuri ya Platini aliyoifanya kati ya 1998 na 2002 wakati alipokuwa mshauri wa ufundi wa Blatter.

Kwa nyakati tofauti jana, baadhi ya wadau wa soka nchini walielezea hukumu hiyo ya kamati ya maadili ya Fifa.

Aliyewahi kuwa katibu mkuu wa TFF, Angetile Osiah alisema Tanzania inapaswa kujifunza kutokana na uhuru wa vyombo vya Fifa katika kutoa uamuzi kwa maendeleo ya soka la Tanzania.

“Kwangu ni uhuru wa chombo kilichomwondoa, yaani kamati ya maadili,” alisema Osiah na kuongeza, “Hii ndiyo kamati aliyoiunda (Blatter), lakini kutokana na vyombo vya Fifa kufanya kazi kwa uhuru, vimemchunguza na kumkuta na hatia ya ufisadi huo.

“Hivi ndivyo vitu tunapaswa kujifunza kwamba ukiteuliwa na rais wa TFF, haimaanishi kuwa hutakiwi kufanya uamuzi asioupenda, bali unafanya uamuzi kwa masilahi ya mpira,” alisema Osiah.

Kocha wa Taifa Stars, Charles Mkwasa alibainisha kuwa kama kweli vigogo hao wa soka duniani wamepatikana na hatia hiyo ni haki yao kufungiwa.

Aliyekuwa mwenyekiti wa Chama cha Soka Tanzania (FAT), hivi sasa TFF, Alhaji Muhidin Ndolanga alisema kwa kosa la rushwa viongozi hao walistahili kufungiwa kutojihusisha na masuala ya soka maisha yao yote.

Kipa wa zamani wa Taifa Statrs, Kitwana Manara alisema kuwa kifungo cha vigogo hao wa soka duniani kimebainisha msimamo wa Fifa na ndiyo unaofaa kuigwa hata Tanzania.