Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wasaudia wajiondoa kwa Salah

Muktasari:

  • Hii sio mara ya kwanza timu za Saudia kuingia katika harakati za kutaka kumsajili Salah na baadae kuachana naye

Liverpool,England. Staa wa Liverpool na timu ya taifa ya Misri, Mohamed Salah ataendelea kubaki Liverpool hata baada ya dirisha la usajili la Januari, kutokana na kujiondoa kwa klabu za Saudi Arabia katika vita ya kutaka kumsajili.

Awali ilionekana wazi kuwa Salah ataondoka Anfield Januari kuelekea Mashariki ya Kati, lakini uwezekano huo umepungua katika wiki za hivi karibuni tangu aripotiwe kumaliza tofauti zake na benchi la ufundi na mabosi wa  Liverpool, alilolishutumu kwamba halimtendei haki na linataka limbebeshe mzigo wa lawama.

Salah ana mkataba wa kuendelea kuitumikia Liverpool  hadi Juni 2027, na anakunja takribani Pauni 350,000 kwa wiki, mshahara ambao ulidaiwa kuwa huenda ukaongezeka kufikia mara tatu ikiwa angetua Saudia.

Imeripotiwa kuwa shauku ya klabu kubwa za Saudi imepungua, kwa kuwa zinaona kuna nafasi ndogo ya kumpata katika dirisha la usajili la Januari.

Awali iliripotiwa kuwa klabu za Saudia ambazo ni Al-Hilal, Al-Qadisah na Neom zilikuwa zinamwinda  Salah na kuwa tayari kutoa pesa nyingi ili kumsajili na kumlipa mshahara.

Hata hivyo, licha ya nia yao ya kumsajili kupungua kwa sasa, kuna uwezekano zikarudi tena katika harakati kwa siku za usoni, hasa baada ya Mtendaji mkuu wa Ligi ya Saudia, Omar Mugharbel, kuthibitisha mapema mwezi uliopita kuwa “Salah anakaribishwa” katika ligi hiyo.

Hii sio mara ya kwanza timu za Saudia kuingia katika harakati za kutaka kumsajili Salah na baadae kuachana naye, iliwahi kutoka mwaka 2023 ambapo Al-Ittihad iliwasilisha ofa ya Pauni 150 milioni ambayo ilikataliwa na Liverpool.

Akizungumza kuhusu tetesi za Salah, baada ya ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Wolves, Desemba, 27, kocha wa Liverpool, Arne Slot alijaribu tena kupoza mjadala kuhusu mustakabali wa Salah. Alisema:

“Nilipomjumuisha kwenye kikosi dhidi ya Brighton, hiyo ilikuwa ni ishara kwamba tulikuwa tumemaliza tofauti zetu. Kwa sasa yuko AFCON na wana michezo muhimu kule, kwa hiyo ni haki kwake na timu ya Misri kuwa na utulivu, hivyo  tusizungumzie sana habari zake hapa linapokuja suala la Liverpool."