Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Winga mpya atua Yanga, KenGold yashtua

Muktasari:

  • Usajili wa staa huyo raia wa DR Congo umeilazimisha Yanga kuachana na aliyekuwa mshambuliaji wake, Jean Baleke ili kukidhi mahitaji ya wachezaji 12 wa kimataifa kwenye timu hiyo.

Yanga imekamilisha usajili wa mshambuliaji anayemudu pia kucheza winga wa kushoto, Jonathan Ikangalombo kutoka AS Vita, lakini taarifa ni kwamba nyota huyo atacheza mechi za ndani tu za Ligi Kuu na Kombe la Shirikisho (FA), kutokana na awali kuichezea Vita kimataifa, huku usajili wa KenGold ukishtua.

Yanga imemsajili mchezaji huyo kwa mkataba wa miaka miwili akiwa anatajwa kuwa mmoja kati ya wachezaji wenye kasi, lakini mwenye uwezo wa kucheza nafasi kadhaa uwanjani.

Usajili wa staa huyo raia wa DR Congo umeilazimisha Yanga kuachana na aliyekuwa mshambuliaji wake, Jean Baleke ili kukidhi mahitaji ya wachezaji 12 wa kimataifa kwenye timu hiyo.

Ikangalombo amejiunga na Yanga kwa mkataba wa miaka miwili ambapo muda mchache kabla dirisha la usajili halijafungwa alitambulishwa kwenye mitandao rasmi ya klabu hiyo ukiwa ni usajili wa pili wa timu hiyo kwenye dirisha dogo lililofungwa juzi baada ya awali timu hiyo kumsajili beki Israel Mwenda  akitokea Singida Black Stars.

Ikangalombo mwenye miaka 22, alitumika kwenye mechi za awali Kombe la Shirikisho akiwa na AS Vita ambayo hata hivyo, ilitolewa kwenye michuano hiyo mwanzoni akicheza winga ya kushoto kwenye michezo miwili.

Yanga Jumapili itakuwa kwenye Uwanja wa Mkapa kuikabili MC Alger mchezo ambao umeshika hatma ya timu zote mbili kufuzu hatua inayofuata kutokana na kila moja kuwa na nafasi na winga huyo hatakuwa sehemu ya kikosi hadi msimu ujao kama timu yake itapata nafasi ya uwakilishi.

Kuhusu suala la Baleke ambaye awali iliripotiwa kuwa aligoma kujiunga na Namungo kwa mkopo, inaelezwa kuwa anataka klabu hivyo ivunje mkataba wake ili aondoke na kwenda kutafuta changamoto nyingine baada ya kutumika kwenye timu hiyo kwa miezi sita tu na kufanikiwa kufunga bao moja.

Kwenye dirisha lililofungwa juzi, KenGold ndiyo ilionekana kushtua  zaidi baada ya kufanya usajili wa wachezaji 24 wakiwemo wakongwe Bernard Morrison 'BM', Obrey Chirwa, Erick Kabamba na Stephen Sey.

Wengine ni Zawadi Mauya aliyewahi kutamba na Kagera Sugar, Yanga na Singida BS, Emanuel Asante (Namungo), Mubashid Seidu (Ghana), Kyala Lassa (Zambia), Elnest Kwofie (Ghana), Kelvin Yondani, Mohamed Yusuph (Dodoma Jiji), Mathias Juviliani, Nassir Bofu, Abdul Abdulai , Thompson Unachi (Nigeria), Maulid Mbegu, Sele Bwenzi, Joseph Ambokege, Ahmed Chambela, Sadala Lipangile

Sandale Komanje, Rojas Gabriel 'Jigwa', Fredrick Kalubunga kutoka Vipers.

Pia ikiwa inatarajiwa kuwa muda wowote itamtambulisha kocha Vladslav Heric raia wa Serbia aliyekuwa akiinoa klabu ya Venda ya Afrika Kusini akipita pia timu mbalimbali ikiwamo Chippa Utd, Cape Town na Free State Stars.

Azam yenyewe imefanya usajili wa wachezaji wawili Zouzou Landry (AFAD Djekanou), Zidane Sereri (Dodoma Jiji) huku ikiwaondoa Yannick Bangala (AS Vita Club), Adam Adam (TZ Prisons), Franklin Navarro (Haijafahamika).

Kwa upande wa Simba ambayo haikuwa bize sana, ilimsajili Elia Mpanzu pekee huku ikiwaondoa Ayoub Lakred na Salehe Karabaka.

Fountain Gate imewasajili  Said Mbatty (Huru), Shabani Pandu Hassan, Mudrik Abdi Shehe, 'Gonda' (JKU), Jackson Shiga, Cosmas Lucas (Coastal Union), Mtenje Albano (Dodoma Jiji), Kassim Haruna 'Tiote' (Huru), Daniel Joram 'Gustavo', Kelvin Nyanguge (Pamba FC), Ibrahim Parapanda, Nassor Kapama (Kagera Sugar), Paulo Godwin Ulomi (Mwembe Makumbi City).

Huku Pamba ikiwasajili Deus Kaseke (Huru), Habib Kyombo, Hamad Majimengi, Mohamed Kamara, Abdoulaye Yonta Camara (Singida Black Stars), Mathew Tegisi Momanyi (Shabana FC), Rally Bwalya (Napsa Stars FC), Shassiri Nahimana (Bandari FC), Cherif Ibrahim (Coton Sport FC), Zabona Mayombya (TZ Prisons), Abalkassim Suleiman (Fountain Gate).

Singida Black Stars imewasajili Frank Assinki (Inter Allies FC), Jonathan Sowah (Al-Nasr Benghazi), Hussein Masalanga, Morice Chukwu (Tabora United), Eliuter Mpepo (Huru).

Waliosajiliwa Namungo ni Salehe Karabaka (Simba), Daniel Amoah (Huru), Derrick Mukombozi (Huru), Najim Mussa (Singida BS), Emmanuel Charles (Kagera Sugar), Issa Abushehe 'Messi' (KVZ FC), Joshua Ibrahim (KenGold), Anderson Solomon (Dodoma Jiji).

Kwa upande wa  Kagera imewasajili Edmund John (Singida BS), Omary Buzungu (Mtibwa Sugar), Moubarack Amza (Namungo FC), Saphan Siwa (Tusker FC).

Walioingia Coastal Union ni Amara Bagayoko (ASKO de Kara), Raphael Daud, Mizar Kristom (Namungo FC), Vitalis Nkosi (Fountain Gate).

Kwa upande wa Tabora ikawasajili, Jean-Noel Amonome (AS Arta/Solar7), Yassin Mustapha (Huru), Fikirini Bakari (Fountain Gate), Joseph Akandwanaho (Mbarara City), Emmanuel Mwanengo (FK Vakhsh Bokhtar).

Dodoma jiji ikasajili wawili ambao ni Mukrim Issa 'Miranda' (Coastal Union), Abdi Banda (Baroka FC).

Tanzania Prisons imewasajili Adam Adam (Azam), Rabbin Sanga (Singida Black Stars), Amade Momade (Namungo), Athuman Sufian Mwemfua (Junguni Utd), Yusuph Athuman (Huru), Gustapha Saimon (Dodoma Jiji).

Mashujaa ikawachukua Danny Lyanga (JKT TZ), Yahya Mbegu (Singida Black Stars), Emmanuel Martin (Dodoma Jiji). JKT Tanzania ikasamsajili Ally Msengi (TZ Prisons).

Huku KMC ikiwasajili watatu Ahmed Bakari Pipino (Magnet Academy), Deusdedith Okoyo (Huru), Shaaban Idd Chilunda (Huru).