Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Yanga Princess yaivua Simba ubingwa Ngao ya Jamii, ikitinga fainali

Muktasari:

  • Msimu uliopita, Yanga Princess ilipoteza mechi mbili za Ligi Kuu ya wanawake dhidi ya Simba Queens pamoja na mechi moja ya nusu fainali ya Ngao ya Jamii.

Dar es Salaam. Yanga Princess imetinga hatua ya fainali ya Ngao ya Jamii ya Ligi ya Wanawake baada ya kuifunga Simba Queens kwa mikwaju ya penalti 4-3 kwenye nusu fainali ya pili ya mashindano hayo iliyochezwa katika Uwanja wa KMC Complex, Dar es Salaam.

Matokeo hayo sio tu yameifanya Yanga Princess itinge fainali bali pia yameivua Simba Queens ubingwa ambao ilikuwa inaushikilia wa mashindano hayo.

Dakika 90 za mechi hiyo zilimalizika kwa sare ya bao 1-1 na hivyo refa wa mechi hiyo Amina Kyando kuamuru mikwaju ya penalti itumike kusaka mshindi wa mchezo huo.

Yanga Princess ndio ilikuwa ya kwanza kupata bao la mapema dakika ya kwanza kupitia kwa Agnes Pallangyo aliyeunganisha kwa kichwa mpira wa krosi wa Adebisi Ameerat ambao ulianzia kwenye kona fupi ambayo ilianzishwa na wachezaji wake.

Bao hilo lilidumu hadi katika dakika za lala salama za mchezo huo ambapo Simba ilisawazisha kupitia kwa Jentrix Shikangwa  akimalizia mpira uliookolewa vibaya kwa kichwa na Danai Bobo wa Yanga.

Baada ya filimbi ya mwisho kupulizwa na refa Kyando, shujaa wa Yanga alikuwa ni kipa Rita Akarekor aliyeokoa penalti tatu za Simba Queens na kuifanya timu yake iibuke na ushindi kwenye mechi hiyo.

Katika nusu fainali ya kwanza, JKT Queens iliibamiza bila huruma Ceasiaa Queens baada ya kuifunga mabao 7-0.

Aliyeiongoza JKT Queens kutembeza dozi hiyo alikuwa ni mshambuliaji Stumai Abdallah ambaye akipachika mabao manne yeye mwenyewe (hat trick) katika dakika za 45, 46 na 65 huku mabao mengine matatu yakifungwa na Winfrida Gerard, Janet Matulanga, Yasinta Mitoga na Anastazia Katunzi.

Winfrida Gerard alianza kuipatia JKT Queens, bao la kwanza katika dakika ya 20 na Mitoga akafunga katika dakika ya 44, Katunzi akifunga katika dakika za nyongeza za kipindi cha kwanza na Janet Matulanga ndiye aliyehitimisha ushindi huo mnono wa timu yake akipachika bao katika dakika ya 87.

Hii ni mara ya pili kwa mashindano ya ngao ya jamii kwa wanawake kufanyika nchini ambapo mara ya kwanza ilikuwa ni msimu uliopita ambapo Simba Queens ilitwaa ubingwa kwa kuifunga JKT Queens kwa mikwaju ya penalti 5-4 baada ya timu hizo kutoka sare ya bao 1-1 katika dakika 90 za muda wa kawaida.

Fainali ya Ngao ya Jamii kwa wanawake imepangwa kuchezwa Jumamosi, Oktoba 5 katika Uwanja huohuo wa KMC Complex ambapo itatanguliwa na mechi ya kuwania mshindi wa tatu.A